Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Septemba 19, 2025 ameungana na waombolezaji katika Misa Takatifu ya Mazishi ya Masista wa shirika la Wakarmeli Wamisionari wa mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu Boko Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Akitoa Salaam za Pole wakati wa Misa Takatifu ya Mazishi, RC Chalamila amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia anatoa pole kwa shirika na kanisa Katoriki kwa ujumla kufuatia vifo hivyo ambavyo vilitokana na ajali ya gari pia Mkuu wa Mkoa ametoa pole na rambirambi ya shilingi milioni 10 pamoja na kuchangia milioni 10 nyingine kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kanisa la Parokia hiyo ya Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu. "Miili hii ya Masista ni pengo kubwa kwa Kanisa Katoriki na Shirika la Wakarmeli Wamisionari wa Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu, Tuyapokee yote katika Kristo kama Biblia ilivyosema" Alisema RC Chalamila
Ifahamike kuwa Masista hao 4 ambao ni Sr M. Lilian G Kapongo, Sr. M.Nerina De Simone, Sr. M. Damaris Matheka, Sr Stellamaris Muthini walifikwa na umauti Septemba 15,2025 kutokana na ajali ya gari lililogongana na gari kubwa Mkoani Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa