Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametangaza kutoa zawadi ya shilingi milioni 20 pamoja na viwanja viwili kwa timu ya Taifa la Tanzania (Taifa Stars) mara baada ya kufunzu hatua ya robo fainali huku akiahidi motisha zaidi kulingana na matokeo ya mchezo wa leo dhidi ya Morocco.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Agosti 22, 2025 RC Chalamila amesema kila bao litakolofungwa katika mchezo huo litazawadiwa shilingi milioni 5 ambapo mfungaji atapokea milioni 1 na mtoa pasi ya bao (assit) atapokea shilingi laki 5.
Aidha amebainisha kuwa kipa atakayefanikisha kuzuia bao bila kuruhusu nyavu zake kuguswa atajinyakulia zawadi ya gari jipya aina ya Toyota Crown.
Zawadi hizi ni ishara ya heshima kubwa kwa Taifa Stars kwa kuendelea kutuwakilisha vizuri, nawashukuru kwa kushinda michezo 3 mfululizo. "Nawasihi watanzania kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Benjamini Mkapa kushangilia timu yetu" Alisema RC Chalamila
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa