Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka viongozi na watendaji katika Mkoa huo kubuni na kutekeleza miradi yq maendeleo ambayo itaweka historia au alama isiyosahaulika kwa jamii, kuhakikisha wanafanya majukumu yao kwa weledi ili waache athari chanya za maendeleo pindi wanapomaliza muda wao au kuhama kituo cha kazi ili waweze kukumbukwa kwa mazuri
Akizungumza katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano maalum uliokutanisha watendaji wa Halmashauri ya Temeke ambapo Halmashauri hiyo imewasilisha taarifa ya miradi ya elimu na afya inayotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 70 ambapo RC Chalamila ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuandaa mpango huo wenye masilahi mapana kwa wananchi
Aidha RC Chalamila amewasisitiza watendaji hao pamoja na viongozi wa Wilaya zote za mkoa huo chini ya wakuu wa wilaya kuhakikisha waakwenda sambamba na maono ya Rais Dkt Samia kwa kuimarisha huduma muhimu za kijamii na amesisitiza watendaji na viongozi kuacha kumbukumbu nzuri za kazi walizozifanya wanapomaliza vipindi vyao vya utumishi
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ametolea mfano wa msongamano wa magari jijini humo kama moja ya changamoto inayowakabili wananchi wa jiji hilo na kusema ni muhimu kubuni mpango wa kumaliza changamoto hiyo jambo ambalo litakumbukwa daima
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda amesema katika miradi hiyo ya shule na ya afya inayotekelezwa kupitia mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na 2026/2027 miradi yote inatekelezwa kwa mfumo wa ghorofa ili kuepuka changamoto ya uhaba wa maeneo
Mpango huo uliowasilishwa unahusisha shule tatu za Makangarawe,Mwmbebamia na Kibondemaji,lakini pia unahusisha hospotali mbili za vigoa na malela pamoja na stendi ya mbagala
Mwisho RC Chalamila amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha kila Halmashauri Mkoani humo inaanzisha timu ya mpira, pia zianzishwe Sports Academy vilevile ameelekeza kwa majengo mapya ya shule yanayojengwa sasa yawe na Smart Classes ili kwenda sambamba na ulimwengu wa kidijitali
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa