-Asema ni muhimu kuelewa vizuri mfumo wa uboreshaji Kaya masikini sambamba na taaluma ya ujasiriamali ili kuepuka kutumia pesa bila kuzalisha.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Machi 12, 2025 katika ukumbi wa mikutano Arnatoglo wakati akizindua zoezi la malipo ya Ruzuku kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini wanaoishi katika nyumba za kupanga kando ya barabara ya mabasi ya mwendo kasi (BRT)
RC Chalamila amesema uzinduzi wa malipo hayo kwa walengwa wa TASAF unalenga kusaidia wakazi wa mjini kunufaika na fursa za kiuchumi zinazoletwa na BRT kwa kupunguza gharama kubwa za kuishi pembeni ya njia za mabasi yaendayo haraka.
Mpango huu unasaidia Kaya masikini ambazo ziko katika hatari ya kushindwa kumudu kuishi karibu na njia ya BRT kutokana na kuongezeka kwa gharama ya maisha kunakosababishwa na uwepo wa BRT na pia unalenga kusaidia wakazi wa mjini wenye kipato cha chini kunufaika na fursa za kiuchumi zinazotokana na uboreshaji wa usafiri kupitia mfumo wa mabasi yaendayo haraka.
Hata hivyo RC Chalamila baada ya kuwakabidi fedha wanufaika hao amewataka kuwa na matumizi sahihi ya fedha hizo, " Ni lazima kuelewa mfumo mzima wa uboreshaji kKaya maskini sambamba na taaluma ya Ujasiriamali ili kuepuka kutumia pesa hizo bila kuzalisha, kwa mfano umeshapokea fedha unakwenda kufungua genge ili uzalishe zaidii " Alisema Chalamila.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa