-Asema bado bajeti zinazotengwa kwenye taka na uchafu ni kidogo sana
-Ataka hatua za haraka zifanyike katika kupendezesha Jiji la Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 10,2024 ameongoza kikao cha kimkakati cha wadau cha udhibiti wa suala la maji taka na uhifadhi wa mazingira katika ukumbi wa Arnautoglo Mnazimmoja Jijini humo
RC Chalamila akiongea wakati wa kikao hicho amesema masuala ya uchafu yanayatesa majiji mengi Duniani pamoja na wataalam au viongozi kwenda kujifunza maeneo mbalimbali lakini utekelezaji unakuwa hafifu hivyo ni wakati muafaka kila mmoja kuamka sasa masuala ya usafi yawe ni tabia na utamaduni wa kila siku
Aidha RC Chalamila amesema masuala ya uhifadhi wa mzingira yapewe kipaumbele katika Taasisi na wilaya zote za mkoa huu ambapo amesema bado bajeti zinazotengwa kwa ajili ya taka na uchafu ni kidogo sana hivyo ni vema kufanya maboresho ya kibajeti.
Vilevile RC Chalamila ametaka hatua za haraka kuchukuliwa katika kupendezesha jiji ikiwemo kuweka Perving, kupanda maua na bustani maeneo mbalimbali ya Mkoa pia kupaka rangi majengo chakavu ili DSM ivutie wakati wote Sanjari na hilo
RC Chalamila amekemea vikali magari kupaki ovyo barabarani ambapo amesema sio kila sehemu unaweza weka kituo cha magari ila ofisi inawezekana amewataka wakuu wa wilaya kusimamia hilo pia amesema suala la kudhibiti taka linaweza kutoa fursa za ajira kwa vijana ambao siku zote wanatafuta ajira hivyo ni vema kuwa na ubunifu katika hilo
Kwa upande wa katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt Toba Nguvila ambaye ndiye mtendaji mkuu katika Mkoa amemuhakishia Mkuu wa Mkoa kuyafanyia kazi maagizo na maelekezo yake kwa masilahi mapana ya wana Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla Mwisho kikao kazi hicho kimewahusisha wadau na wataalam kutoka katika Taasisi, na wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa