Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila Februari 8,2025 amesaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Aga Khan IV ambaye alifikwa na umauti Februari 4, 2025 akiwa na umri wa miaka 88.
Ifahamike kuwa Aga Khan IV amekuwa na mchango mkubwa katika Taifa la Tanzania hususani katika Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na uwekezaji wake mkubwa kwenye Sekta ya Afya kupitia Hospitali yake maarufu kwa jina la Hospitali ya Aga Khani ambayo imekuwa ikitoa matibabu ya kibingwa kwa jamii.
Hivyo kupitia uwekezaji huo Aga Khan IV ataendelea kukumbukwa na watanzania siku zote.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa