Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amefanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa shule mpya wilayani Temeke na kujiridhisha juu ya taarifa iliyowasilishwa na Halmashauri hiyo juu ya ujenzi wa miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 70 ambayo ujenzi wake umeanza
Akizungumza akiwa katika mradi wa ujenzi ya shule ya Sekondari Mwembe bamia wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam RC Chalamila amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia katika utekelezaji wa miradi ya elimu lengo ni kuhakikisha kila mtoto aliye kwenye umri wa kusoma anapata fursa hiyo
RC Chalamila amesema kuwa maamuzi yaliyochukuliwa na Halmashauri hiyo kujenga miradi kwa fedha za ndani zaidi ya shilingi bilioni 70 ni maamuzi magumu yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi huku akisisitiza suala la ujenzi wa miradi ya shule na hospitali kufanywa kwa mfumo wa ghorofa kutokana na ufinyu wa Ardhi
Aidha akizungumza wakati akifanya majumuisho ya ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema ujenzi unaofanyika ni fedha iliyotolewa na Rais inayotokana na watanzania pamoja na vyanzo vingine ambavyo Rais amekuwa akivitafuta akijitoa katika kuwahudumia na kuwatumikia watanzania
Hata hivyo ametumia ziara hiyo kuwakumbusha watanzania kujitokeza kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushiriki kupiga kura Oktoba 29,2025 ili kuwezesha kupata viongozi watakaoiongoza Tanzania kwa miaka mingine mitano kwa njia za kidemokrasia
Naye Nasoro Sultani Matope ni mmoja wa wananchi wakazi wa Mwembebamia waliojitokeza wakati wa ziara hiyo ameipongeza Serikali chini ya Rais Dokta Samia kwa kuleta miradi hiyo ya shule ambayo inakwenda kumaliza changamoto ya watoto wao kusafiri umbali mrefu kwenda shule
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa