-Asema Viongozi wa Dini ni muhimili muhimu katika kulinda Amani ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Taifa amani na kuhubiri masuala ya amani na utulivu wa Nchi ili kuepuka madhara yatokanayo na uvunjifu wa amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu
Akizungumza leo jijini Dar es salaam latika kikao maalum na viongozi wa Dini RC Chalamila amesema viongozi wa dini ni muhimili katika kutunza amani ya nchi huku akisisitiza kuwa serikali kupitia jeshi la polisi itaendelea kuimarisha ulinzi na amewataka watanzania kujifunza madhara ya uvunjifu wa amani kupitia mataifa jirani yenye vurugu
Aidha RC Chalamila ameongeza kuwa hakuna kiongozi anaependa kuona wananchi wake wakikabiliwa na vitendo vya ukatili na uvunjifu wa amani hivyo ni muhimu kwa viongozi wa Dini kusimama imara kupitia madhabahu kwenye nyumba za ibada kuhubiri amani
Kwa upande wa Shekh wa Mkoa wa Dar es Salaam ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya amani ya Mkoa huo Shekh Walid Kawambwa amesema viongozi wa Dini wana nafasi kubwa ya kuimarisha amani na kujenga maadili ndani ya jamii hivyo watumie nafasi zao vizuri huku Mtume Boniface Mwamposa wa makanisa ya Arise and Shine akihimiza viongozi wa Dini kutumia vyema madhabahu kuhubiri amani
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo amesema kuwa viongozi wa dini wamekuwa na mchango mkubwa katika kuombea amani na utulivu wa nchi kwa kushirikiana na makundi mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara na bodaboda
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa