Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amekabidhi magari mawili aina ya Land Cruiser Prado yaliyotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuwawezesha wakuu wa wilaya ya Kigamboni na Ubungo kuwafikia wananchi na kuwahudumia huku pia akikabidhi gari moja aina ya Crown kwa golikipa wa Timu ya Taifa ya Tanzania Yakoub Suleiman kutokana na kazi nzuri aliyofanya kuzuia magoli kwenye mashindano ya CHAN
Akizungumza Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kukabidhi gari hizo hafla ambayo imefanyika katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Mkuu RC Chalamila amesema magari hayo yametolewa na Rais Dokta Samia ili wakuu wa wilaya waweze kuwafikia wananchi kwa urahisi kuwahudumia na kutatua changamoto za wananchi
Aidha Chalamila amemkabidhi Golikipa wa timu ya Taifa ya Tanzania Yakoub Suleiman gari aina ya Crown ikiwa ni ahadi aloyoitoa kwenye mchezo wa robofainali ya mashindano ya CHAN kati ya timu ya Taifa ya Tanzania na Morocco ambapo amesema licha ya kufungwa golimoja golikipa huyo alifanya kazi nzuri
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila ametumia hafla hiyo kuzitaka halmashauri zote za mkoa huo kuwa na timu za mpira zinazomilikiwa na Halmashauri na pamoja na kuwa na viwanja vya michezo mbalimbali ikiwemo ngumi ili michezo iwe ni fursa ya kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando mara baada ya kupokea gari hiyo amemshukuru Rais kwa kuwawezesha kupata usafiri wa utakaosaidia kuwahudumia wananchi hivyo ameahidi kuimarisha huduma kwa wananchi huku Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akiahidi kuendelea kuimarisha michezo wilayani humo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa