-Ataka mashirika hayo kulinda amani ya taifa letu
-Amuagiza Katibu Tawala wa Mkoa Kufuatilia mashirika yote kujua utendaji wake wa kazi
-Asistiza umuhimu wa mashirika hayo kufanya kazi kwa kuzingatia utamaduni wa kitanzania
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 20,2025 amefungua Mkutano wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanafanya kazi ndani ya Mkoa huo katika ukumbi wa Maktaba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
RC Chalamila akifungua mkutano huo amesema anatambua kazi nzuri inayofanywa na mashirika hayo kwa kushirikiana na Serikali hivyo ni muhimu kuendelea kulinda amani iliyoko ili kuendelea kufanya kazi hizo kwa uhuru na amani " Kamwe tusiige kinachofanywa nchi zingine kwa sababu amani ikitoweka hatuna Tanzania nyingine au Dar es Salaam nyingine kila mmoja awe sehemu ya kulinda amani iliyoko" Alisema RC Chalamila.
Aidha RC Chalamila amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila kuhakikisha anafuatilia mashirika yote ambayo usajiri wake uko Dar es Salaam kujua utendaji wake wa kazi kwa kuwa Mkoa ndiyo una mashirika mengi zaidi ukilinganisha na mikoa mingine ya Tanzania kwa takwimu za sasa Mkoa una mashirika takribani 3030 hivyo ni vizuri kujua yanafanya nini kwa masilahi mapana ya ustawi wa watu wetu.
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa ameyataka mashirika hayo kufanya kazi zake kwa kuzingatia utamaduni wa kitanzania ili yasiwe sehemu ya umomonyoko wa maadili na vitendo vingine viovu katika Taifa hususani katika Mkoa huu.
Mkutano unalenga kuboresha na kuimarisha ushirikiano kati ya mashirika hayo na Serikali pia kukumbushana sheria na miongozo mbalimbali ili kuwa na mashirika yenye tija kwa umma
Mwisho Mkutano huo umehudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila, wataalamu wengine kutoka Sekretarieti ya Mkoa, wadau mbalimbali pamoja na viongozi wa mashirika yasiyo ya Kiserikali kutoka Wilaya zote za Mkoa huo yaani Ilala,Kinondoni, Ubungo, Kigamboni na Temeke
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa