Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 4,2025 amefungua kongamano la mawakili wanawake lililoandaliwa na chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) kwa kushirikiana na chama cha wanasheria wanawake Tanzania (TWLA) katika ukumbi wa TLS Wakili House kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
RC Chalamila amepongeza Jukwa la mawakili wanawake (women Lawyers Forum) kwa kuwa kupitia jukwa hilo wanawake hupata fursa za kukutana, kujadili masuala mbalimbali ambayo yana athari za moja kwa moja katika taifa letu hasa kundi kubwa la wanawake nchini.
"Kongamano hili la tofauti ambalo lina umuhimu mkubwa sana kuelekea uchaguzi mkuu tarehe.29 Octoba 2025 ambapo haki na usawa wa kijinsia na maendeleo ya taifa letu vinakwenda kuamuliwa na wananchi " Alisema RC Chalamila
Aidha RC Chalamila ameeleza mafanikio ya Serikali kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi ambapo amesema Serikali imeendelea kusema na kutenda katika kuimarisha nafasi ya mwanamke katika sekta za ushiriki wa uongozi, huduma za kisheria na mfumo wa haki kama vile uteuzi wa viongozi wanawake, uteuzi wa majaji Wanawake, na kuanzisha mifumo jumuishi ya Haki.
Vilevile RC Chalamila amesema amefahamishwa kuwa bado kuna changamoto ambazo wanawake ambao ni sehemu ya TLS, TAWLA na jamii kwa ujumla wanazipitia hivyo amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwa mshirika wao mkuu ili kuhakikisha mazingira salama na yenye usawa wa kijinsia, ambapo amewasihi TLS na TAWLA kuendelea kuwa nguzo imara ya ushirikiano, muunganisho naushawishi kwa serikali, jamii na taasisi za kimataifa ili kuleta chachu ya kimaendeleo nchini
Kongamano hili ni fursa ya kuimarisha mapambano, kuunda mitandao mipya na kujiimarisha kimaadili na kivitendo akisisitiza RC Chalamila
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa