-Ni katika kikao Cha Robo ya tatu kati yake na Wakuu wa Sehemu na Vitengo-Mkoa, Wakurugenzi na Wakuu wa Sehemu na Vitengo- Halmashauri
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila Leo tarehe 15 Mei, 2025 amefanya kikao Cha Robo ya tatu ya mwaka na Wakuu wa Sehemu na Vitengo- Mkoa, Wakurugenzi, Wakuu wa Sehemu na Vitengo- Halmashauri katika Wilaya ya Ubungo ambapo jumla ya maagizo 14 yametolewa naye
Kwanza, amekemea ujenzi wa majengo usiofuata taratibu, ujenzi wa maeneo ambayo hayapaswi kujengwa ambapo wengine hujenga mpaka ghorofa ndefu na kupelekea kuwachungulia viongozi pia maeneo mengine hayatakiwi maghorofa unakuta yanajengwa hivyo amewaagiza Wakurugenzi, Wahandisi kusimamia taratibu na Sheria za ujenzi na kutokutoa vibali bila Sheria na taratibu za ujenzi kufuatwa
Pili, Dtk. Nguvila amekemea tabia za kumbi za starehe kupiga sana kelele huku zingine kupiga kelele katika maeneo ya makazi ya viongozi na wananchi kupelekea kushindwa kupata utulivu hivyo ameagiza Wakurugenzi kulifanyia kazi pia hili
Tatu, Katibu Tawala amewaagiza Wakurugenzi, Maafisa Uchaguzi kuhamasisha wananchiKujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ambalo kwa Dar es Salaam zoezi la kujiandikisha linatarajiwa kuanza tarehe 16 Mei mpaka 22 ,2025
Nne, RAS Nguvila Amewataka Maafisa Mipango kuwa na Takwimu sahihi vichwani mwao kwani wao ni watu wa kutoa Takwimu hizo mara kwa mara kwenye kazi zao
Tano, Dkt. Nguvila amewaagiza Wakurugenzi kuhakikisha miradi yote isiyokamilika kukamilika na kuanza kufanya kazi mara Moja, miradi hiyo ya madarasa, Vituo vya afya, na masoko
Sita, Katibu Tawala amewaagiza Wakurugenzi kusimamia Suala la asilimia kumi ipasavyo na kuhakikisha wanaopata asilimia kumi ni wale makundi lengwa.
Saba, RAS Nguvila amewaagiza Wakurugenzi kusimamia utekelezaji wa Biashara saa 24 na kusema ni jambo linawezekana kabisa kwani limeshaanza kufanya kazi baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na kuipongeza Ubungo kwa uzinduzi mkubwa pia
Nane, Katibu Tawala amewaagiza Wakurugenzi kupambana katika kuyainua mapato katika Halmashauri zao huku akitaka malengo ya kukukusanya mapato kutimia maana vyanzo vya ukusanyaji huo vipo hivyo kuwataka kuongeza watenda kazi
Tisa, Dkt. Nguvila ameeleza Kuhusu Uongezeko la majimbo yaliyopitushwa na Tume Ya uchaguzi kuwa ni Jimbo la Chamazi na Kivule hivyo kuwataka Wakurugenzi kuongeza nguvu ya usinamizi
Kumi, RAS Nguvila amewaagiza Wakurugenzi kuongeza usimamizi wa utekelezaji wa Miradi ya kimkakati na katika utekelezaji huo, taarifa za ubia kati yao lazima kwanza zipitie kwa Katibu Tawala kabla ya Kwenda TAMISEMI
Kumi na Moja, Katibu Tawala amewaagiza Wakurugenzi kujiridhisha na miradi itakayopendekezwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru kwani tunajiandaa kukimbiza Mwenge katika Mkoa wetu
Kumi na Mbili Dkt. Nguvila ameeleza uwepo wa mitungi ya Gas ipatayo 1000 kutoka Taifa Gas na kuwaagiza Wakurugenzi ifikapo ijumaa ya wiki ijayo kuichukua na kuwafikishia walengwa
Kumi na Tatu, RAS Nguvila amewaagiza Wakurugenzi kusimamia matumizi ya Mfumo wa Pepmis na pipmis na kusema ni ya lazima na yeyote asiyetekeleza hili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake
Kumi na Nne, Katibu Tawala ameagiza madeni ya watumishi na wakandarasi kulipwa na kusema pesa inayokusanywa itengwe na ilipe watumishi na wakandarasi ili wafanye kazi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa