-Ukusanyaji wa Mapato
-Kuzingatia Maslahi ya Watumishi
-Uhamasishaji uendelee wa watu kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Abdul Rajabu Mhinte ameyaseme hayo Leo tarehe 18 Agosti, 2025 katika kikao chake na Wakuu wa Sehemu na Vitengo kutoka Sekretarieti ya Mkoa, Wakurugenzi na Wakuu wa Sehemu na Vitengo kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjeee Hall
Mosi, RAS Mhinte amesisitiza suala la Ukusanyaji wa Mapato ambapo amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo kuweka nia thabiti katika hili ili kufikia malengo yaliyowekwa na hata kuyavuka. *"Hili ni jukumu la msingi kabisa linalotupa nguvu ya kuendelea kuwahudimia wananchi"* Alisisitiza RAS Mhinte
Pili, Katibu Tawala Aliwasihi Viongozi hao kuzingatia Maslahi mbalimbali ya Watumishi ambapo alisema sisi Viongozi wajibu wetu Mkubwa ni kwenda kuwahudimia vema watumishi wetu. Mambo ya madai mbalimbali ya watumishi yaendelee kushughulikiwa ikiwa ni pamoja na kumalizwa kabisa ili nao wajisikie wako kazini na kutimiza wajibu wao ipasavyo, vile vile tuwapime utendaji kazi wao kwa wakati sahihi ili nao wapate Stahili zao husika
Tatu RAS Mhinte amepongeza wingi wa watu uliojitokeza kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na akasisitiza hamasa zaidi ziendelee kufanyika ili watu wajitokeze kwenda kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025
Ikumbukwe kuwa katika kikao hicho Cha Robo ya Nne ya Mwaka 2025, mambo mengi mazuri yalijadiliwa na kufikia muafaka na kilichobakia ni utekelezaji
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa