Katibu Tawala Mkoa Bi Rehema Madenge aliyeketi wa pili kulia akiwa na Maafisa Maendeleleo wa Halmashauri baada ya kufunga mafunzo ya viongozi wa Majukawaa ya Uwezeshaji wanawake kiuchumi
Katibu Tawala Mkoa Bi Rehema Madenge aliyeketi wa pili kulia akiwa na Viongozi wa Majukwaa baada ya kufunga mafunzo hayo
-Awataka Viongozi wa majukwa ya Uwezeshaji wanawake kiuchumi DSM kushuka hadi ngazi ya Kata na mitaa kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa wanawake
-Aagiza Maafisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri kuwasaidia wanawake kutumia fursa ya mikopo ya 10%
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi Rehema Madenge amesema Mama akiwezeshwa Kiuchumi Sehemu kubwa ya Taifa imewezeshwa kwa kuwa akina mama ndio wanaosimamia familia kwa sehemu kubwa hakuna mama anayeweza kutekeleza familia yake, mama ni nguzo, hata hivyo kwa mujibu wa Sensa 2022 imeonyesha wanawake ni wengi zaidi kuliko wanaume hivyo ni wakati muafaka wa Wanawawake kujikwamua Kiuchumi kwa Masilahi mapana ya jamii na Taifa
Katibu Tawala Mkoa ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Viongozi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala Boma.
Aidha amewataka Viongozi wa Majukwaa ya Kuwezesha wanawake kiuchumi kushuka katika ngazi za Kata na Mitaa kuwajengea uelewa wanawake kutumia fursa zilizoko ili kukuza Uchumi wao na jamii kwa Ujumla.
Vilevile ameelekeza Maafisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri kutumia maarifa waliyonayo kuwasaidia wanawake kukuza kipato hususani kutumia fursa ya mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri za Manispaa Katika maeneo yao.
Ifahamike kuwa uhuishaji wa majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Dar es Salaam umeshaanza wanawake watumie fursa hiyo kujiandikisha fomu zinapatikana katika Kata zote za Mkoa wa DSM
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa