• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

DC SOPHIA MJEMA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MASUALA YA HUDUMA YA MAJI KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM

Posted on: August 30th, 2017

HOTUBA YA MHESHIMIWA PAUL MAKONDA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ILIYOSOMWA NA MKUU WA WILAYA YA ILALA MHESHIMIWA SOPHIA MJEMA KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO WA WADAU WA MASUALA YA HUDUMA YA MAJI KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM NEW AFRICA HOTEL 30 AUGUST 2017.

 

Katibu Tawala (M) na Watumishi kutoka Sekretariate ya Mkoa wa DSM,

Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dsm,

Wakurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Temeke , Ubungo, Kigamboni na Kinondoni,

Mkurugenzi Mkuu DAWASA na DAWASCO,

Wadau wa Maji na Wadau wa Maenedeleo Mkoa wa DSM,

Watumishi wa DAWASA na DAWASCO,

Ndugu Wananchi, Waandishi wa Habari,

Mabibi na Mabwana,

Ninafuraha kubwa kuwa hapa leo hii kushiriki nanyi katika kikao hiki muhimu cha Wadau wa Maji na Usafi wa Mazingira katika Mkoa wetu wa Dar es Salaam. Kama alivyoeleza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, kikao hiki nilitaka kifanyike mara tu baada ya kumaliza Maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Maji Mwezi Machi mwaka huu 2017 ambapo niliwaagiza watendaji wa Sekta ya Maji wafanye maandalizi ya kikao hiki. Lakini watendaji walioko chini ya Ofisi yangu walinishauri nifanye kwanza ziara ili kuona maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya majisafi na majitaka katika Mkoa wetu. Nami nilikubaliana nao na nikafanya ziara hizo kama ambavyo Katibu Tawala amefafanua.

Ndugu Washiriki wa Kikao, katika ziara nilizofanya  nilitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kupitia Mamlaka ya maji, DAWASA. Katika ziara hiyo niliweza kujifunza mambo mengi sana kuhusu mipango mbalimbali ya Serikali inayoendelea hivi sasa ya kuwapatia Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam huduma ya maji.  Niliona jitihada kubwa zinazofanywa na Mamlaka ya Maji ya DAWASA za kusimamia miradi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya Majisafi katika Jiji letu. Pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali yetu kupitia Mamlaka ya DAWASA nimegundua bado kuna mapungufu  mengi na malalamiko mengi kuhusu huduma ya maji kwa wananchi wetu.

Hivi sasa maji yanayozalishwa ni mengi sana ambayo yanaweza kukidhi zaidi ya asilimia 90 ya Wananchi wote lakini ukweli ni kwamba maji hayo bado hayajafika kwa Wananchi kutokana na uhaba wa mtandao wa mabomba hususan ni maeneo yaliyoendelezwa miaka ya hivi karibuni na yale yaliyoko pembezoni mwa Jiji.

Ndugu Washiriki wa Kikao, Kufuatia changamoto nilizoziona katika ziara yangu na kupitia mikutano niliyofanya maenneo mbalimbali ya Jiji ndio maana nikaamua niwaite Wadau mbalimbali ili tujadili kwa pamoja namna ya kuzikabili changamoto hizi ili tuweze kuendana na malengo ya Serikali ya kuhakikisha kuwa asilimia 95 ya wananchi wanapata huduma ya maji ifikapo mwaka 2020.

Lakini kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ambapo maji yanayozalishwa hivi sasa ni mengi sana kukidhi zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji; ndio maana mimi na wataalamu wangu tukasema kuwa wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam wanaweza kupata huduma ya Majisafi na salama wote (100%) ifikapo 2020 “HUDUMA YA MAJI MKOA WA DAR ES SALAAM KWA WOTE IFAKAPO 2020” iwapo tutakaa na Wadau wote kuona namna bora na ya ufanisi wa kuyasambaza maji yote  yanayozalishwa hivi sasa.

Leo tumekutana na baadhi tu ya Wadau wetu wa Maendeleo ambao wamekuwa wanatusaidia sana katika suala zima la kuhakikisha tatizo la maji linapungua.

Ndugu Washiriki wa Kikao, Napenda kutoa shukrani za pekee kwa wadau wetu WaterAid kwa kufadhili kikao hiki. Aidha, napenda pia kuwashukru wadau mbalimbali bila kuwasahau Benki ya Dunia na Korea ya Kusini ambao wamekubali kufadhili miradi mikubwa ya maji na usafi wa mazingira Katika Jiji la Dar es Salaam. Aidha, natambua kuwa Wadau wote walioshiriki hapa na ambao wameshindwa kushiriki siku ya leo najua wanatambua kuwa wananchi wa Dar es Salaam wana kiu ya huduma na wote kwa pamoja tunapaswa  kuhakikisha kuwa wanapata huduma bora ya maji. Kwa juhudi zenu za kusaidia katika upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa Mkoa wetu. Kwa pamoja nawaomba tuzidi kushirikiana katika kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira ili kuhakikisha kuwa malengo tuliojiwekea yanafikiwa kwa wakati.

Ndugu Washiriki, Ni matumaini yangu kuwa kwa siku hii ya leo tutapata fursa ya kuelewa na kushiriki katika mijadala ya namna ya kukabiliana na changamoto za utoaji wa huduma ya Maji. Nina imani kubwa sana kuwa Mkutano huu utatoa maazimio ambayo yatakuwa suluhu ya matatizo ya maji katika Jiji letu.

Baada ya kusema hayo natamka rasmi kuwa Mkutano wetu umefunguliwa rasmi.

Asanteni kwa kunisikiliza naomba sasa tuendelee na RATIBA. 

MAJI NI UHAI NA USAFI WA MAZINGIRA NI UTU 

“HUDUMA YA MAJI MKOA WA DAR ES SALAAM KWA WOTE IFIKAPO 2020”







Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa