• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

Posted on: May 23rd, 2025

 

Na. Mwandishi wetu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Maafisa Habari  Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Seriksali za Mitaa kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.

Waziri Mchengerwa ametoa wito huo leo, wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Ofisi ya Rais-TAMISEMI kinachofanyika katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma uliopo kwenye Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma.

“Mmebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi hivyo msiwaache watanzania walishwe habari potofu” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa amesema kuwa, Maafisa Habari nchini ni rasilimaliwatu muhimu hivyo wakitambua wajibu wao na kujiimarisha kiutendaji ni wazi kuwa wananchi watapata taarifa sahihi kwa wakati.

“Iwapo kila mmoja wenu akiwa mzalendo na kutambua wajibu wake, habari mtakazozitoa ndio zitaaminiwa na kupokelewa na watanzania kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambayo imeshamiri hivisasa,” Waziri Mchengerwa amehimiza.

Waziri mchengerwa amesema, ana amini kwamba maafisa habari waliopo wana weledi na ujuzi unaowawezesha kutoa taarifa sahihi zenye tija kwa wananchi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Sanjari na hilo, Waziri Mchengerwa ameelekeza Maafisa Habari wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa washiriki kwenye ziara za viongozi ili wapate uelewa utakaowawezesha kutangaza kwa ufanisi mafanikio ya Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha, Waziri Mchengerwa amewaelekeza waajiri katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha Maafisa Habari wanaokaimu ukuu wa vitengo ambao wana sifa, wapewe vitengo ili waweze kutekeleza kikamilifu jukumu la kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi zao ikiwa ni pamoja na kutangaza mafanikio yaliyopatikana kwenye eneo la utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambalo limepewa kipaumbele na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Ukatili Kinara Migogoro inayohitaji Msaada wa Kisheria-Waziri Mkuu

    June 16, 2025
  • Wananchi Dar Kunufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia

    June 14, 2025
  • RC Chalamila, Samia Legal Aid Kuzinduliwa Juni 16, 2025 DSM

    June 13, 2025
  • Wataalam Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Wakutana na Kamati ya Usalama ya Mkoa-DSM

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa