KIKAO CHA WADAU WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI AWAMU YA TATU (TASAF III) KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM CHAMALIZIKA LEO TAREHE 30/06/2017 KWA MIKAKATI MIKUBWA KUWEKWA YA NAMNA YA KUWAHUDUMIA WALENGWA WA MPANGO.
Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa tarehe 28-30 Juni, 2017 na kuhudhuriwa na Waratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, Wahasibu wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini, Maafisa Ufuatiliaji (TMO),Wafuatiliaji wa Utimizaji wa masharti ya Afya na Elimu (Maafisa Afya na Elimu Msingi na Sekondari) na Wataalamu wa Ngazi ya Mkoa.
Katika siku ya kwanza wadau hao wa mpango wa kunusuru kaya masikini walipata mafunzo ya mfumo wa malipo kwa njia ya Ki-ilekroniki “Electronic Payment System” ambapo walipata kuelewa kuwa mbali na malipo ambayo hufanyika kwa njia ya kawaida ya kupewa pesa mikononi lakini kuna njia nyingine za kutumia simu au akaunti zao za benki kuingiziwa pesa. Njia hii itasaidia walengwa wa mpango kupata malipo yao moja kwa moja wakiwa katika maeneo yao ya Makazi bila kwenda kwenye maeneo ya malipo.
Katika Siku ya pili, Wadau walijifunza umuhimu wa kuhuisha taarifa za walengwa kwa kila Halmashauri kwenye mfumo wa Tasaf ambapo hapa walielezwa kuwa kila mlengwa asipohuishiwa taarifa zake hawezi kupata huduma stahiki hivyo kukosa kipato,fedha ya chakula,elimu na huduma za afya pia. Vilevile Wadau walihimizwa kuwa takwimu ndiyo nyenzo muhimu zitakazowasidia Watendaji na Wadau wengine kupima uelekeo wa Mpango huu.
Siku ya tatu wadau walipata fursa ya kujikumbusha maana halisi ya Mpango wa Kunusuru kaya maskini, lengo lake,walengwa wa mpango huo ni watu gani, changamoto katika utekelezaji wa mpango huo na kuweka maazimio ya namna ya kutatua changamoto hizo.
Katika kufunga Mkutano huo Mwenyekiti aliyeteuliwa na wadau hao katika kikao kazi hicho Bw. Hermeni J. Msia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa dhati wadau hao kwa kuhudhuria katika kikao kazi hicho kwa muda wa siku tatu bila kukosa na kuweza kujua mbinu mbalimbali za kwenda nazo katika kuwaahudumia walengwa vilevile aliwasisitizia wadau kwenda kufanya kazi kwa bidii bila kujali changamoto zilizopo kwani mpango huo wa kusaidia kaya masikini umefanya mambo makubwa na ya muhimu kwa Taifa kama vile:-
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa