-Amshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa imani yake kwake.
-Aahidi kuendeleza yale yote mazuri ya mtangulizi wake Dkt Toba Nguvila.
-Dkt Toba Nguvila ataka Sekretarieti ya Mkoa kumpa zaidi ushirikiano Katibu Tawala Bwana Abdul Mhinte.
Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Toba Nguvila amemkabidhi rasmi ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa huo bwana Abdul Rajab Mhinte leo Julai 9,2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa Makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na Sekretarieti ya Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri zote tano, Makatibu Tawala wa Wilaya na maafisa Tarafa, Dkt Toba Nguvila amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kumuamini na kumpatia nafasi ya Katibu Tawala wa Mkoa na kisha kuridhia ombi lake la kwenda kuanza mchakato wa kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Makete, vilevile ameshukuru Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila kwa ushirikiano aliokuwa akimpatia katika kipindi chote alichohudumu pamoja na ushirikiano alioupata kutoka kwa watumishi wote wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo ametoa rai ushirikiano huo uendelee tena zaidi kwa Katibu Tawala mpya bwana Abdul Mhinte.
Aidha Dkt Toba Nguvila amesema yako mengi sana ya kukabidhiana kwa kifupi amempitisha maeneo kadha ya kufanyia kazi kama vile Ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa, maandalizi ya uzinduzi wa soko la Kariakoo, mfuko wa barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam, Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mkoa Kigamboni, Biashara saa 24 pamoja vikao vya robo vinavyohusisha taasisi za umma katika Mkoa huo.
Vilevile Dkt Toba Nguvila amesema makabidhiano hayo ni ya kawaida katika utumishi ambapo alitoa historia yake kwa ufupi hivyo kubadilisha vituo ni jambo la kawaida anachomba kwa watumishi wote ni kuendelea kumuombea dua ili afikikie matamanio ya dhamira yake ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Makete Mkoa wa Njombe.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa bwana Abdul Rajab Mhinte baada ya kukabidhiwa ofisi ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii tena kwa ushirikiano mkubwa na wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watumishi wote ili kwenda sambamba na dhamira ya Mhe Rais Dkt Samia ya Kuwaletea Wananchi Maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa