Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Abdul Rajabu Mhinte pamoja na Madaktari wasio na mipaka (Medecins Sans Frontieres/Doctors Without Borders ) Leo tarehe 03 Septemba, 2025 wamesaini makubaliano ya usaidizi wa utoaji wa huduma za Dharura katika Mkoa wa Dar es Salaam ambao watashirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Amana, kituo Cha Afya Magomeni na Buguruni hasa maeneo ambayo Yana idadi kubwa ya wakazi na yenye viashiria vikubwa vya uhitaji wa huduma za Afya za Dharura.
Ushirikiano huo utajumuisha kuwajengea uwezo watoa huduma za Afya katika kukabiliana na majanga pamoja na magonjwa ya mlipuko
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madaktari wasio na mipaka Ndg. Tommaso Santo ameishukuru Serikali ya Tanzania na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kukubali kusaini makubaliano hayo, kusaidia kuwajengea uwezo watoa huduma, kutoa vifaa tiba na vile vile kushiriki katika majanga au magonjwa ya mlipuko yatakayotokea katika Mkoa wa Dar es Salaam
Ikumbukwe kuwa Katibu Tawala aliwashukuru wadau hao na kuwahimiza kuendelea kusapoti juhudi za Serikali katika kuhakikisha huduma za Afya za Dharura na kukabiliana na majanga zinakuwa Bora. *"Mkoa wa Dar es Salaam usisahaulike licha ya kusapoti maeneo mengine kwa sababu ya wingi wa watu ambao wanahitaji huduma hizi pale Dharura zinapotokea, Alisisitiza RAS Mhinte"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa