- Wamkabidhi Vifaa vya kuzolea TAKA pamoja na fyekeo " Slasher"
Katika Kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa DSM Mhe Amos Makalla ya SAFISHA, PENDEZESHA DAR ES SALAAM Kampuni ya GNM CARGO imemkabidhi RC Makalla vifaa vya kuzolea taka na mafyekeo kwa lengo la kuongeza NGUVU katika kufanikisha kampeni hiyo.
Akiongea wakati anakabidhiwa Vifaa hivyo RC Makalla amewashukuru kwa GNM kuwa wadau wa kwanza kuotoa mchango wao toka azindue Mkakati wa Usafi na Uhifadhi wa Mazingira DSM
RC Makalla amesema mpango huu wa USAFI ni endelevu jamii itambue usafi unaanza na mtu binafsi, Kaya na hatimaye usafi wa pamoja ambao Utafanyika mara moja kila mwisho wa mwezi kuanzia saa 12:00 hadi 3:00 Asubuhi.
Aidha RC Makalla ameendelea kutoa rai kwa wadau wengine kuiga mfano wa GNM CARGO kuunga mkono Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM
"Dar es Salaam ni Mkoa Mkubwa ambao ni lango lakini pia kuna wawekezaji wengi na fursa nyingi hivyo ni vema kuweka Mkoa safi na Mandhari nzuri ya kuvutia" Alisema RC Makalla
Kwa Upande wa Afisa masoko GNM Ndg Amin Mahava amemhakikishia RC Makalla kuendelea kushirikiana na Ofisi yake kwa maslahi mapana ya Wananchi wa DSM pia amemkabidhi Tishet 2 kwa ajili ya Mazoezi
USAFI UNAANZA NA WEWE, SHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA USAFI WA PAMOJA DISEMBA 4, 2021 KIVUKONI-ILALA DSM
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa