Shirika la GAIN kupitia mradi wa kuwezesha masoko kuzalisha katika hali ya Usalama KFMW leo wamefanya kikao na Wadau katika Ukumbi wa Lecam Social Hall Buguruni Ilala- Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa Kikao hicho Meneja wa mradi Ndg Edwin Josiah amesema Kikao kilikuwa na lengo la kuwasilisha matokeo ya tafiti zilizofanyika juu ya mtazamo wa wauzaji na wanunuzi katika masoko hususani Soko la Buguruni kuhusu Usalama wa Chakula ( Safe food ) Sokoni.
Aidha Bwana Edwin amefafanua kabla ya kikao hicho wamepata wasaa wa kutembelea na kujionea Uhalisia kwa sasa katika Soko la Buguruni na kuongea na wafanyabiashara kusikia maoni na ushauri, hivyo kikao kilichofanyika kimetoa fursa kwa wadau kwa pamoja kujadili namna bora ili kufikia adhima ya Usalama wa Chakula katika Masoko likiwemo Soko hilo.
Kwa upande wa Meneja wa Soko hilo Ndg Seleman mfinanga amesema Shirika la GAIN wamekua mdau mzuri katika kufikia Usalama wa Chakula katika Soko la Buguruni kwa kufadhiri Ukarabati mkubwa wa Soko kuanzia kuweka Sakafu, kuezeka paa sehemu ya kina mama lishe, Kuboresha sehemu ya mchinjio ya kuku, Kuwapa majiko ya gesi kwa kina mama lishe ili waachane na matumizi ya mkaa, hapo awali Soko lilikuwa katika hali isiyofaa kwa Usalama wa Chakula kulikuwa na tope Kipindi cha mvua, vibanda havikuezekwa lakini kwa sasa Soko liko katika Mazingira mazuri hivyo tunawashukuru sana Shirika la GAIN
Mwisho Kikao kazi hicho kimehudhuliwa na Wataalam toka Wizarani ,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Ofisini ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Viongozi wa Soko la Buguruni, wafanyabiashara na Wataalam kutoka Shirika la GAIN ( Global Alliance for Improved food Nutrition)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa