
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba ameridhia ujenzi wa Kituo cha Daladala Bunju B, Kata ya Mabwepande Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam ambapo ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.3.
Akiongea wakati wa ziara aliyoifanya leo Disemba 29, 2025 wakati akitembelea Soko la Bunju B pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi, waziri Mkuu amesema kuwa amepokea wazo la uhitaji wa ujenzi wa Kituo cha daladala na ameahidi kuwa hitaji la fedha kiasi cha shilingi Bilioni 2.3 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa stendi hiyo haraka itapatikana.
"Nakubaliana nanyi na naunga mkono ujenzi wa Stendi hii kwani itakwenda kuongeza kasi na mzunguko wa Biashara katika eneo hili la Bunju B" Alisema Dkt Mwigulu.
Sanjari na hilo amesisitiza kuwa kituo hicho cha daladala ujenzi wake utakwenda sambamba na miundombinu ya Barabara, Soko na Maduka ili kuwa na mzingira rafiki ya Kibiashara ambayo yatapelekea kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumala na ndiyo dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan


Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa