-Zaidi ya walimu 1000 kupanda Treni ya Umeme ya SGR kwenda Hifadhi ya Taifa Mikumi-Morogoro
-Lengo ni kuunga mkono Juhudi za Mhe Rais Dkt Samia kufuatia
uwekezaji mkubwa alioufanya katika usafiri wa reli ya SGR
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 30,2024 akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala boma ametoa taarifa kwa umma juu ya uzinduzi wa Treni ya SGR ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoani Dodoma Agosti 01,2024
Akiongea mbele ya waandishi wa habari RC Chalamila amesema ofisi yake imeandaa Safari SGR Mikumi Tour kwa walimu wa Mkoa huo, ambayo inatarajiwa kufanyika Agosti 02,2024 siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kufanya uzinduzi wa SGR Mkoani Dodoma
Aidha RC Chalamila amesema program hiyo inaanza kufanyika kwa kundi la walimu Zaidi ya 1000 na itaendelea kufanyika kwa makundi mengine kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dkt Samia kutokana na utekelezaji wa kishujaa wa mradi mkubwa wa SGR ambao unakwenda kurahisisha na kuweka rekodi ya kihistoria na mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri wa reli ndani ya nchi na nje ya nchi hususani barani Afrika.
RC Chalamila ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za kishujaa zinazofanywa na Mhe Rais katika Nyanja mbalimbali hapa nchini ili kumtia moyo ambapo amesema katika tukio la kukata utepe katika mradi wa SGR akiwa Dar es salaam wanachi wajitokeze kwa wingi.
Mwisho Safari ya SGR Mikumi TOUR kwa walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni ya Siku 2 Siku ya kwenda Ijumaa Agosti 02,2024 na Siku ya Kurudi Jumamosi Agosti 03,2024 ambapo msafara utaanzia Stesheni kuu ya SGR-DSM.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa