• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

Posted on: May 23rd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wauguzi nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kwa kufuata misingi ya sheria ya kazi yao ili kulinda afya za wananchi na kwamba Serikali Mkoani humo inatambua na kuthamini kazi ya uuguzi katika kulinda afya za wananchi

Akizungumza leo Mei 23,2025 Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya wauguzi kimkoa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema wauguzi ni nguzo muhimu kwenye utoaji wa huduma za afya hivyo ni muhimu kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu kama ambavyo kanuni za kazi hiyo zinavyowataka

Aidha RC Chalamila ameitaka jamii kutambua na kuthamini kazi inayofanywa na wauguzi na kusisitiza kuwa Serikali Mkoani humo itaendelea kushirikiana na wizara ya afya ili kuimarisha zaidi mazingira ya utolewaji wa huduma za afya, pia akiisisitiza jamii kuendelea kutambua sera ya afya inayohitaji wananchi kuchangia huduma hiyo

Sanjari na hayo amesisitiza wakazi wa jiji hilo na watanzania kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa mujibu sheria kwani kodi ndio nyenzo ya kuboresha huduma za kijamii ikiwemo  huduma za afya na amemshukuru Rais Dokta Samia kwa namna ambavyo amekuwa akiimarisha upatikanaji wa huduma za Afya hivyo amesisitiza kuwa wauguzi ndiyo faraja kubwa kwa wagonjwa

Kwa upande wake Rais wa chama cha Wauguzi Tanzania Tanna Ezekiel Henry amewataka wauguzi kuendelea kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kufuata sheria na kanuni za kazi hiyo huku akiitaka jamii kuheshimu kazi ya uuguzi kwenye kulinda afya za wananchi

Kwa upande wake Rais wa chama cha wakunga Tanzania TAMA Dokta Beatrice Mwilike amezungumzia umuhimu wa ushiriki wa wanaume kwenye Afya ya mama mjamzito wakati wa kujifungua na kwamba wanaendelea kuimarisha mafunzo kwa wakunga ili kuboresha huduma huku Kaleb Kiula Muuguzi kutoka hospitali ya Mloganzila wakati akisoma risala ameiomba Serikali kudhibiti kazi za baadhi ya wasanii wanaodhihaki kazi ya uuguzi.

Maadhimisho hayo yamebeba kaulimbiu isemayo "Wauguzi Nguvu ya Mabadiliko Duniani"ambapo kupitia maadhimisho hayo wauguzi wamewasha mshumaa wa upendo na kula kiapo cha kufanyakazi kwa uadilifu na kutunza siri mbele ya mkuu wa Mkoa


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa