Vyama vya Ushirika huanzishwa na kuandikishwa kwa kuzingatia Sheria ya Ushirika ya Mwaka 2003. Mkoa una jumla ya Vyama vya Ushirika 879 vilivyoandikishwa vikiwemo Vyama vikuu vya Ushirika (Unions) vitatu (3) ambavyo ni Chama Kikuu cha Ushirika cha Mazao (DARECU), Chama Kikuu cha Viwanda (TICU) na Chama Kikuu cha Akiba na Mikopo (SCCULT) Ltd. Pia kuna vyama vitano (5) vya Ubia (Joint Venture Enterprises).
Hadi kufikia mwezi Desemba 2013, Mkoa ulikuwa na jumla ya Vyama vya Ushirika vya Msingi 871 vilivyo andikishwa kisheria; ambapo Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) ni 662, Vyama vya mazao (korosho) 23, na Vyama 186 vya aina nyingine kama vile ujenzi wa Nyumba, Viwanda, Biashara, Usafiri na Uvuvi.
Vyama vya Ushirika hapa Mkoani vina jumla ya wanachama 208,233 hadi mwezi Desemba 2013, kati yao, SACCOS zina wanachama 193,930.
Wanachama katika SACCOS wamenunua Hisa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 10.8, pia wameweka Akiba na Amana zenye thamani ya Shilingi Bilioni 108.67 hadi Desemba 2013. Mikopo iliyotolewa kwa wanachama hao hadi Desemba, 2013 ni ya thamani ya Shilingi Bilioni 226.5
Mkoa kupitia Maafisa Ushirika wake umeweza kufanya ukaguzi na usimamizi wa Vyama na kutoa ripoti kwa Wanachama wake kwa Vyama 352 kati ya Vyama vilivyo hai 652 hadi Desemba 2013 sawa na asilimia 54.% ya Vyama ambavyo ni hai.
Moja ya jengo la chama cha ushirika -WANAMA SACCOS
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa