TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA KATAZO LA MIFUKO MILAINI YA PLASTIKI KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM KWA MWAKA 2021.
UTANGULIZI
Mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya Wilaya tano za Utawala ambazo ni Ilala Kinondoni , Kigamboni Temeke na Ubungo na Mkoa una jumla ya Halmashauri 5 ambazo ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Manispaa za Kinondoni , Kigamboni , Temeke na Ubungo ambazo zina wakazi wanakadiriwa kuwa 5.2 m kwa mwaka 2020 na ongezeko la watu la asilimia 4.6 kwa mwaka .
Kazi ya kutoa Elimu ya kuacha Matumizi ya Mifuko milaini kama vibebeo.
Baada ya Tamko la Waziri la Tarehe 8 Januari 2021 Mkoa wa Dar es Salaam ulianza kutoa Elimu kwa wakazi na Wafanyabiashara kuacha kuzaliasha kusambaza kuuza na matumizi ya Mifuko milaini ya plastiki kama vibebeo bali itumike kama vifungashio.
Mkoa uliunda kikosikazi cha kutoa Elimu kwa wananchi na wafanyabiashara kwa kufanya ukaguzi katika masoko na maduka.
Mkoa ulikagua Mabucha ya kuuza nyama na samaki yapatayo 58 katika Manispaa ya Ubungo na Mabucha 105 katika Jiji la Dar es Salaam kwa kutoa elimu ya kuacha matumizi ya mifuko milaini kubebea Nyama .
Aidha Mkoa ulifanya ukaguzi na kutoa Elimu kwenye Masoko 22 katika masoko ya Mkoa katika Halmashauri zote tano kama inavyoonyeshwa hapo chini.
Kikosikazi kazi kilifanya ukaguzi katika Masoko ya mkoa kama ifutavyo
Jina la Halmashauri
|
Jina la Soko lililokaguliwa.
|
Hali halisi
|
Jiji la Dar es Salaam
|
Buguruni , Ilala , Karikaoo , Vingunguti Mchikichini (5)
|
Bado matumizi ya Mifuko milaini inatumika kubebea bidhaa za sokoni kama vile karoti , pilipili ,njegere vitunguu n.k
Soko la Kariakoo ndio wazalishaji na wauzaji wa Roller za Kutengeneza Mifuko hii |
Manispaa ya Ubungo
|
Mburahati Manzese, Mabibo, Simu 2000 , Shekilango na Makaburini Sinza (6)
|
Matumizi ya Mifuko Milaini yapo kwa kiasi kidogo kwa kufungia bidhaa za sokoni kama vile karoti , pilipili ,njegere vitunguu n.k
|
Manispaa ya Temeke
|
Temeke sterio , Tandika , Tazara na Mbagala rangi tatu (4)
|
Matumizi ya mifuko yapo kwa kutumika kama vibebeo katika Saoko la Mbagala na kufungia Barafu na ice cream
|
Manispaa ya Kinondoni
|
Tandale , Mtambani , Magomeni , Tegeta na Makumbusho (5)
|
Matumizi ya Mifuko Milaini yapo kwa kiasi kidogo kwa kufungia bidhaa za sokoni kama vile karoti , pilipili ,njegere vitunguu n.k
|
Manispaa ya Kigamboni
|
Soko la Ferry na Kwa Urassa (2)
|
Hakuna matumizi makubwa ya mifuko milaini na Masoko haya ni madogo sana
|
|
|
|
Elimu ilitolewa kwa wafanyabishara Bucha matumizi ya mifuko milaini kama vibebeo na itumike kwa mujibu ya maelekezo ya TBS
Aidha kila Manispaa imendelea na kutoa elimu na kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali katika maeneo yao kama ifuatavyo
Jina la Halmashauri
|
Eneo lilokaguliwa
|
Hali halisi
|
Jiji la Dar es Salaam
|
Ukaguzi umefanyika katika soko la Kariakoo , Buguruni, Ilala na vingunguti na Mchikichini .Aidha ukaguzi umefanyika katika Kiwanda kinachozalisha mifuko hii eneo la gongo la mboto .
Matangazo ya gari yanapita mitaani kuwaarifu wananchi kuhusu katazo la mifuko milaini ya plastiki kama vibebeo. |
Inakadiriwa jumla ya kilo 300 zimekamatwa katika kiwanda cha Gongo la Mboto na kiasi cha kgs 260 zimekusanywa katika masoko ya Mchikichini, Ilala na Buguruni Mifuko iliyokusanywa ipo makao Makuu ya Jiji na Ofisi ya Kata Mchikichini na Deport ya Mazingira Kamata .
Jumla ya faini ya tshs 500,000 zimekusanywa kwa Jiji |
Manispaa ya Ubungo
|
Elimu imetolewa kwenye masoko ya Mburahati, Mabibo, simu 2000 Manzese na Shekilango
|
Ukaguzi umefanyika na Jumla ya Kgs 8 katika soko la mabibo zimekusanywa pamoja na Faini ya kiasi cha Tshs 120,000 na Kgs 13.80 zimekusanywa Katika soko la Mbezi Msigani Pamoja na Faini ya tshs 130,000 ambapo plastiki zilizokusanywa zimepelekwa NEMC.
|
Manispaa ya Temeke
|
Matangazo yamefanyika kutumia magari kutoa elimu kwa wananchi kuacha matumizi ya mifuko milaini kama vibebeo
|
Ukaguzi umefanyika katika soko la Tandika mnamo tarehe 23.4.2021na jumla ya Kgs 204.22 na jumla ya faini ya tshs 160,000 zimekusanywa katika Manispaa ya Temeke.
|
Manispaa ya Kinondoni
|
Ukaguzi umefanyika katika Maduka na Masoko ya Tandale, Mtambani na Maeneo ya Mwananyamala na Makumbusho
|
Ukaguzi uliofanyika na Jumla ya kgs 9 zimekusanywa katika Soko la Tandale na na kupelekwa NEMC
Mnamo tarehe 23.04.2021 umefanyika katika eneo la Tegeta na jumla ya kgs 2,500 zilikusanywa na faini ya tshs 560,000 |
Manispaa ya Kigamboni
|
Maduka ya wafanyabiashara , soko la feri na soko dogo la kwa Urassa na wauzaji wa jumla na kwenye
Viwanda vya mikate |
Jumla ya Kilo 6 za mifuko zimekusanywa ipo ofisi ya Mazingira. Ukaguzi ulifanyika tarehe 19.04.2021 na tarehe 23.04.2021
Jumla ya tshs |
Hadi kufikia tarehe 30. 04. 2021 jumla ya Kgs 3,293.22 zimekusanywa na jumla ya faini ni tshs 1,740,000 zimekusanywa na kazi bado inaendelea . Kiwanda cha RamsonMoris Company kinaendelea kufutiliwa ili kiweze kurekebisha kasoro na kulipa faini na kupima kiasi cha mifuko iliyokamatwa .
Nawasilishwa .
Valence V. Urassa
AFISA MAZINGIRA
MKOA WA DAR ES SALAAM.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa