Ongezeko la Eneo la Misitu
Ibara ya 31 (f) Kuimarisha sekta ya malisili kwa kuongeza eneo la kupanda miti kutoka hecta 60,000 mwaka 2016 hadi hecta 130,000 mwaka 2020.
Eneo la hifadhi ya misitu ya asili ya kupandwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ni Hekta 4,794 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na Hekta 4,140 kwa mwaka 2016. Ongezeko hili ni hekta 654 sawa na 16%. Ongezeko hilo linatokana na juhudi za Serikali kupanda miti katika maeneo ya misitu iliyoharibiwa na kuongeza eneo la misitu kwa kuwatoa wavamizi waliogeuza misitu kuwa makazi. Hifadhi hizo zinahusisha misitu ya Pwani (Coastal forest Hekta (1,622), Misitu ya Mikoko (3078) na misitu ya kupanda (94).
Upandaji wa Miti
Ibara ya 30 (b) Uimarishaji wa Sekta ya maliasili kwa kuongeza kasi ya upandaji miti kwenye misitu ya jamii ambapo wastani wa miti milioni 200 kwa mwaka imepandwa.
Mkoa unaendelea kuwaelimisha na kuwahimiza wadau mbalimbali kupanda na kuitunza miti katika maeneo yao ili kuboresha mazingira na kupendezesha Jiji. Maeneo yanayopandwa miti ni pamoja na maeneo ya wazi, barabara, makazi, taasisi mbalimbali, viwandani, kandokando ya mito, mabondeni, fukwe za bahari na maeneo ya vyanzo vya maji.
Ili kuweka msukumo katika upandaji miti tarehe 01 Oktoba, 2016, Mkoa ulizindua kampeni ya ‘MTI WANGU’ kwa lengo la kuongeza kasi ya kupanda miti na kuitunza. Katika kipindi hicho miti ipatayo 30,473 ilipandwa. Hadi kufikia mwaka 2018 jumla ya miti 3,503,490 imepandwa kupitia Kampeni ya Mti wangu. kwa kutumia chanzo cha makusanyo ya mapato ya ndani ambapo kiasi cha Sh.52,768,000 zilitumika. Kampeni hii itadumu kwa kipindi cha miaka 4 na lengo ni kupanda miti milioni 4 kufikia mwaka 2019.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa