MALIASILI NA MISITU
Eneo la hifadhi ya misitu la Mkoa kwa sasa ni Ha 4199 kwa mwaka huu 2017 , Ha.3,697 mwaka 2008 ambapo mwaka 2005 ilikuwa ha.588 na mwaka 2000 ha.90 tu. Ongezeko hili linaonyesha kuwa jitihada za kuongeza hifadhi ya misitu katika Mkoa ni kubwa na za kuridhisha.
Kuhusu upandaji miti, Mkoa unaendelea kuwaelimisha na kuwahimiza wadau mbalimbali kupanda na kuitunza miti katika maeneo yao. Katika kuimarisha zoezi hili tarehe 01/10/2016 Mkoa umezindua kampeni ya upandaji miti ijulikanayo kama MTI WANGU. Katika kampeni hii Wananchi katika ngazi ya Kaya wanahimizwa kupanda miti isiyopungua 5 ya matunda na kivuli. Kupitia kampeni hii Mkoa umepanga kupanda miti milioni 4 kufikia mwaka 2019 ili kuboresha mazingira ya Jiji kwa kuongeza Ukanda wa Kijani na kupendezesha Jiji (City greening and beutification). Aidha katika utaratibu huu aina ya miti mbalimbali hupandwa kila mwaka ikiwamo ya matunda, mapambo nishati na biashara. Maeneo yanayopandwa miti ni:- maeno ya wazi, barabara, makazi, taasisi mbalimbali, viwandani, kandokando ya mito, mabondeni, fukwe za bahari na maeneo ya vyanzo vya maji.
SIKU YA UPANDAJI MITI KITAIFA
Kila ifikapo tarehe 01 Aprili ya kila mwaka ni Siku ya Upandaji miti Kitaifa. Mkoa wa Dar es Salaam hufanya maadhimisho haya katika ngazi ya Mkoa. huadhimishwa katika moja ya wilaya kwa mzunguko/zamu kwa kila mwaka ambapo wadau wote hushiriki kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali.
Mwaka 2016/2017 sherehe hizo zilifanyika katika wilaya ya Ilala kata ya Msongola, Shule ya Msingi Yangeyange ambapo jumla ya miti 3000 ya Mijohoro, Miembe, Miharadani na Palm ilipandwa katika siku hiyo ya maadhimisho. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema.
(a) UTEKELEZAJI WA UPANDAJI MITI MSIMU 2016/2017
Lengo la Mkoa lilikuwa ni kupanda miti 1,000,000 kwa kuzingatia utekelezaji wa kampeni ya MTI WANGU ya kupanda miti 4,000,000 kuanzia mwaka 2016 hadi kufikia mwaka 2019 ambapo Manispaa ya Ilala ilipanda miti 16158, Kigamboni 5116, Kinondoni 20,633, Temeke 13,948, Ubungo 14,372. Utekelezaji halisi jumla ya miti 70,227 ilipandwa kimkoa. Mwaka 2015-2016 jumla ya miti 30,473 ilipandwa ambapo Manispaa ya Ilala ilipanda miti 2822, Kinondoni 9100, Temeke 18,557.
Utekelezaji huu wa upandaji miti kimkoa kuanzia 2015/2016, na 2016/2017, jumla ya miti 100,700 imepandwa katika mkoa wa Dar es Salaam.
Halmashauri
|
Idadi ya vitalu
|
Mahali
|
Maelezo
|
Ilala
|
2
|
Kinyamwezi gargden – 1.
|
Kitalu cha mboga, miche ya miti na matunda.
|
Karimjee botanical garden - 1
|
Kitalu cha miche ya miti na maua.
|
||
Kigamboni
|
1
|
Gazaulole
|
Kitalu cha mboga na miche ya matunda
|
Kinondoni
|
Hakuna
|
|
Vilivyopo 3 vimebinafsishwa kwa matumizi mengine ya maeneo hayo. Kitalu kimoja kitaanzishwa katika bustani ya Boko kwa msimu wa 2008/2009.
|
Temeke
|
2
|
Mtoni kwa Azizi Ali garden - 1
|
Kitalu cha miche ya miti, matunda na maua.
|
Temeke
|
1
|
Ofisi ya Wakala wa huduma za misitu veta
|
Kinamilikiwa na wizara ya maliasili na utalii
|
Ubungo
|
hakuna
|
|
Wamepanga kuanzisha ki
|
Jumla
|
5
|
|
|
Halmashauri |
Aina |
Eneo (Ha)
|
Mahali |
Maelezo |
Kinondoni
|
(Miombo) Msitu wa asili wa hifadhi ya pori la akiba la Pande (Pande game reserve)
|
1,223
|
Mabwe Pande
|
Unasimamiwa na Wizara ya maliasili/Utalii.
|
Shamba la miti la Manispaa (msitu wa kupandwa).
|
5
|
Bunju B
|
Unatunzwa na kikundi cha mazingira Bunju.
|
|
|
Hifadhi ya misitu ya Mikoko).
|
189.5
|
Kata za Mbweni, Kunduchi,Ununio, Msasani na Kawe.
|
Inasimamiwa na Wizara ya Maliasili- Idara ya misitu kitengo cha mikoko ikisaidiana na Halmashauri ya Manispaa, CBO`s na vikundi vya mazingira.
|
Misitu ya Kupandwa (watu binafsi).
|
45
|
Mabwe Pande na maeneo mbalimbali.
|
Inamilikiwa na kusimamiwa na watu binafsi.
|
|
Jumla
|
1,462.5
|
|
|
|
Kigamboni
|
Shamba la miti la Manispaa
|
13.6
|
Kata ya Kimbiji na Toangoma.
|
Linasimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
|
Misitu ya kupandwa (watu binafsi)
|
25
|
Kata ya Somangila na Kimbiji.
|
Husimamiwa na kumilikiwa na watu binafsi.
|
|
Misitu ya mikoko.
|
2,500
|
Maeneo ya fukwe za bahari.
|
Inasimamiwa na wizara ya Maliasili – Idara ya Misitu Kitengo cha ikoko ikisaidina na Halmashauri ya Manispaa, CBO`s na vikundi vya mazingira.
|
|
Misitu ya asili
|
36
|
Kata ya Amani gomvu na Somangila
|
Watu binafsi.
|
|
Jumla ndogo
|
|
2574.6
|
|
|
Temeke
|
Mikoko
|
13.2 |
Kata ya Mtoni kijichi
|
Unasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii
|
Mikoko
|
8.3 |
kurasini
|
Unasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii
|
|
Mikoko
|
7 |
kizinga
|
Unasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii
|
|
Jumla Ndogo
|
|
28.5 |
|
|
Ilala
|
Misitu ya asili.
|
13
|
Kitunda
|
Watu binafsi.
|
Shamba la Manispaa
|
5
|
Kinyerezi
|
LInasimamwia na Manispaa.
|
|
Msitu wa mikoko
|
10
|
Daraja la Salenda
|
Inasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwakushirikiana na Manispaa
|
|
Hifadhi ya msitu wa asili wa Zingiziwa.
|
105
|
Chanika
|
Linasimamiwa na Manispaa na vikundi vya utunzaji mazingira.
|
|
Jumla ndogo
|
|
133
|
|
|
|
||||
Jumla
|
Mikoko
|
2728
|
|
|
Jumla
|
Misitu ya kupandwa
|
75
|
|
|
Jumla
|
Misitu ya asili
|
1,395.6
|
|
|
Jumla ya eneo la misitu yote
|
4199
|
|
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa