• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Ilala MC
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA AOKOA BILLION 1.11 KUFUFUA MAGARI MENGINE YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA YALIYOKUFA

Posted on: October 31st, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amekabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya DAR COACH LTD kwa ajili ya kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.

Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 ya Serikali.

RC MAKONDA amesema kuwa Gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya Siku 90 ambapo ameipongeza Kampuni ya DAR COACH LTD kwa kujitolea kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali.

Aidha Mhe. MAKONDA amesema Magari hayo yatafungwa Vifaa vya Kisasa ikiwemo Kiyoyozi (AC), Mfumo wa Chaji ya Simu kila Seat, Runinga, Radio, Viti vya kisasa, Vyoo vya Ndani, Bodi mpya pamoja na mwonekano mzima wa Gari ili ziwe za kisasa.

RC MAKONDA amesema mpango wake wa kuendelea kuongezea nguvu Vyombo vya Ulinzi na Usalama hautokoma kwa kuwa lengo lake ni kuwatumikia Wananchi na Askari wajivunie kufanyakazi chini ya RC MAKONDA.

Amemuagiza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuhakikisha Ving'ora vya Jeshi la Polisi vinakuwa tofauti na kampuni za Ulinzi na Usalama, Magari ya Wagonjwa ili kupunguza Mkanganyiko kwa wananchi na kujengea heshima Jeshi la Polisi.

Katika hatua nyingine amewataka Wanasiasa kufanya Siasa za kistaarabu badala ya kutukana na kutoa lugha chafu kwa Serikali.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na usalama akiwemo Kamanda wa Polisi Dar es Salaam LAZARO MAMBOSASA, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAJAB MWENYUMBU, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. NOEL JAMES ambapo wote kwa pamoja wamempongeza RC MAKONDA.

Matangazo

  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2020 Shule za Sekondari za Serikali December 06, 2019
  • RC Makonda Kuupokea Mwenge wa Uhuru Julai 19 Ukitokea Mjini Magharibi July 18, 2019
  • Rais wa Kongo Kutua Nchini tarehe 13/06/2019 kwa Ziara ya Kikazi na Kupokelewa na Mwenyeji wake Rais Dkt.John Magufuli June 12, 2019
  • Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anawatangazia wananchi wenye Matatizo ya macho kufika kwenye kambi ya macho iliyopo Mtaa wa Hindragand Posta kila Jumamosi na Jumapili kwa kipindi cha Miezi Miwili kupatiwa vipimo,matibabu na miwani bure. October 05, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Afrika Kusini Kutua Nchini Jumatano na Kupokelewa na Rais Dkt John Pombe Magufuli

    August 12, 2019
  • RC Makonda Atoa Mwezi Mmoja kwa Manispaa ya Kinondoni Kuanza Ujenzi wa Fukwe za Coco

    August 09, 2019
  • RC Makonda Azidi Kutimiza Ahadi ya Ufadhili wa Matibabu ya Upasuaji wa Moyo 60 Kutoka Familia Duni

    July 25, 2019
  • RC Makonda Azindua Soko la Kimataifa la Madini na Vito Mkoa wa Dar es Salaam

    July 17, 2019
  • Tazama zote

Video

RC Makonda akiwasilisha utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa