• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Ilala MC
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makonda akabidhi kwa Chama cha Mapinduzi miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwenye Jimbo la Kawe

Posted on: June 30th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara kwenye Jimbo la Kawe kwa lengo la kukabidhi Miradi  iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwa Chama cha Mapinduzi CCM ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizozitoa Rais Dkt. John Magufuli kupitia ilani ya Chama hicho.

Miongoni mwa miradi aliyokabidhi RC Makonda ni Mradi Mkubwa kabisa wa Kuchakata taka wenye thamani ya Bilioni 5.59 uliopo Mwabwepande, Mradi wa Shule Mpya ya sekondari ya Mabwe Tumaini Girls iliyogharimu Shilingi Bilioni 2.6 na Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Kinondoni iliyopo Mabwepande yenye thamani ya Bilioni 2.4.

Aidha RC Makonda amekabidhi pia Mradi wa Matanki makubwa matano na Pampu za kusambaza Maji zilizopo Changanyikeni, Ujenzi wa Kituo cha Afya Bunju chenye thamani ya milioni 600, Mradi wa Makazi ya Askari Mabwepande pamoja na kukabidhi Zahanati ya Mkoroshini kata ya Msasani yenye thamani ya Milioni 408.

Akizungumza katika ziara hiyo RC Makonda amewahimiza wananchi kuhakikisha wanachagua viongozi watakaowaletea maendeleo na sio viongozi wanaopinga kila jambo jema linalofanywa na serikali.

Hata hivyo RC Makonda amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya Kawe ili kusogeza huduma za Afya kwa wananchi wa kata hiyo.

Kesho RC Makonda ataendelea na ziara yake ya kukabidhi miradi kwa Chama cha Mapinduzi CCM kwa upande wa Jimbo la Kinondoni.

Matangazo

  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Serikali - AWAMU YA PILI January 08, 2021
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Kunenge: Stendi Mpya ya Mabasi ya Mbezi Louis Kuanza Rasmi Novemba 30, Majaribio Novemba 25

    November 09, 2020
  • RC Kunenge Afanya Ziara ya Kushtukiza Usiku wa Manane,Atoa Maagizo Mazito kwa Wakandarasi "Wazembe'

    October 17, 2020
  • Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Akutana na Walimu,Awahakikishia kuwa Serikali Itaendelea Kulipa Malimbikizo Yote Wanayodai

    September 22, 2020
  • RC Kunenge Atembelea Miradi na Kutaka Ikamilike kwaWakati

    September 17, 2020
  • Tazama zote

Video

Kampeni ya Tahadhari Dhidi ya Mafuriko kwa Wanafunzi jijini Dar es Salaam
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa