
-Akutana na Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila aanza ziara ya Siku 3 kuanzia leo Disemba 22, 2025.
Naibu Waziri OWM-TAMISEMI Mhe Reuben Kwagilwa ameanza ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Barabara, Afya na Elimu katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Katika ziara yake Mkoani humo alipata wasaa wa kukutana na Mkuu wa Mkoa Mhe Albert chalamila na kufanya mazungumzo ya faragha ofisini kwake Ilala Boma Jijini humo.
Baada ya Mazungumzo hayo akaanza ziara rasmi katika wilaya ya Ilala na Temeke, aikiwa Ilala ametembelea mradi ujenzi wa Shule ya Sekondari ya ghorofa Kutunda relini ambao kukamilika kwake kutagharimu zaidi ya bilioni 7 ambapo amepongeza mradi huo na kuagiza januari 2026 wanafunzi waanze kusoma shuleni hapo.
Vilevile akiwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Kitunda-Kivule- Msongola ameonyesha kusikitishwa na kasi ya ujenzi huo licha ya kuwa tayari Serikali imeshatoa bilioni 4.7 ambapo hapohapo akamuelekeza Mkuu wa wilaya kwa mamlaka aliyonayo kumkamata mkandarasi anayejenga barabara hiyo akahojiwe aje na mpango wa kutekeleza mradi huo kwa haraka hakuna kuongezewa muda ila ni lazima ifikapo April 2026 barabara iwe imekamilika.

Sanjali na hilo akiwa Temeke amefurahishwa na ujenzi wa Shule ya msingi na Sekondari ya ghorofa Mwembe bamia Chamazi pia hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara (Wailes) ambapo amesema ujenzi huo uko nyuma zaidi ya asilimia 36 na mradi huo utagarimu bilioni 21hivyo ameagiza kukamatwa pia kwa mkandarasi kwa ajili ya mahojiano
"Lazima fedha zinazotolewa na Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye miradi zisimamiwe kwa weledi na uaminifu hatutakubali kuchezewa" Alisema Mhe.Reuben.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo amemhakikishia naibu waziri wako tayari kuchapa kazi usiku na mchana kwa masilahi mapana ya Wanachi na ndiyo maono ya Mhe Rais Dkt Samia

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa