Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa leo Disemba 18,2024 amezindua ugawaji wa vifaa vya TEHAMA kwa shule za Sekondari Nchini katika shule ya wasichana ya mchepuo wa sayansi Dar Es Salaam High School, Wilaya ya Ubungo hafla ambayo imehudhuriwa na Mhe Albert Chalamila, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Toba Nguvila, wataalam kutoka TAMISEMI, Wataalam kutoka wilaya ya Ubungo Mhe Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hassan Bomboko, pamoja na viongozi wa chama na Serikali,
Aidha Vifaa vya TEHAMA ni nyenzo muhimu kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia.
Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila akipokea vifaa vya TEHAMA kutoka kwa Waziri wa TAMISEMI kulia Mh Mohamed Mchengerwa mara baada ya uzinduzi huo kwa niaba ya makatibu Tawala wa Mikoa yote ya Tanzania Bara.
Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila kushoto akiteta jambo na Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa