- Kamati iliona ni busara eneo kutumika kwaajili ya ujenzi wa kiwanda Cha Vioo kitakachotoa Ajira kwa zaidi ya Wananchi 6,000 kuliko kutumika kwaajili ya kulaza magari
- Awaelekeza kutafuta eneo lingine watakalolipa Wananchi fidia Ili kujenga Karakana hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA. Amos Makalla amewaelekeza Wakala wa Mabasi ya Mwendokasi DART kuheshimu maamuzi ya kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa iliyotaka wakala hao kutafuta eneo jingine la kujenga Karakana ya mabasi ya Awamu ya tatu kutoka katikati ya mji kuelekea Gongolamboto na kuachia eneo lililokuwa limepangwa kutumika kwaajili ya ujenzi wa kiwanda Cha Vioo kitakachotoa Ajira kwa zaidi ya watu 6,000.
Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makalla kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya BRT Awamu ya tatu ambapo ameshangazwa kuona Wakala hao wanaendelea Kung'ang'ania eneo Hilo licha ya kushiriki kwenye kikao Cha kamati ya Ulinzi na usalama na kuridhia maelekezo Ya kamati.
RC Makalla amesema kikao Cha kamati kiliona ni busara eneo kutumika kwaajili ya kiwanda kitakacholeta tija kwenye uwekezaji, Ajira na kuwezesha Serikali kupata mapato tofauti na kulaza magari.
Kutokana na Hilo RC Makalla amewaelekeza DART kushirikiana na Halmashauri ya Jiji hilo kutafuta eneo lingine watakalolipa Wananchi fidia Ili kujenga Karakana hiyo.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema Tayari *Bank ya Dunia imeridhia kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa kiwanda hicho na tayari Mwekezaji amefanya Maandalizi ya awali eneo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa