
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Disemba 3,2025 amezindua rasmi wodi mpya yenye vifaa maalum vya kisasa kwa ajili ya watoto wachanga kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Jijini Dar es Salaam.
Wodi hiyo inayotoa huduma kwa watoto wachanga inajumuisha wodi ya watoto wachanga (General Ward) Kitengo cha KMC, na chumba maalum cha Kangaroo (Father Care), awali wodi kulikuwa na vitanda 6 tu lakini sasa kina jumla ya vitanda 32 - 15 vya General Ward, 15 vya KMC na 2 vya Kangaroo (Father Care).
Aidha mradi huo ukarabati wake umegharimu jumla ya shilingi za Tanzania 931,992,527 na umetekelezwa kwa awamu mbili ya kwanza mwaka 2020 iligharimu shilingi 349,716,470 na awamu ya pili mwaka huu 2025 iliyogharimu shilingi 582,276,057
Ukarabati huo unaifanya Hospitali ya Amana kuwa miongoni mwa vituo vya huduma bora kwa watoto wachanga nchini Tanzania yenye teknolojia bunifu, matumizi ya takwimu katika kupanga na kuboresha huduma, pamoja na kuimarisha uwezo wa watumishi kupitia mafunzo na ufuatialiaji endelevu.
Vilevile maboresho hayo yamejumuisha ufungaji wa vifaa maalum vya kisasa vinavyotumia teknolojia za kuokoa maisha ambazo ni za msingi kwa uhai wa watoto wachanga waliolazwa, teknolojia hizo ni pamoja na mashine (CPAP) vifaa vya tiba ya mwanga( phototherapy), na vichujio vya hewa ya oksijeni.
Mwisho ifahamike kuwa mradi huo umetekelezwa kupitia mpango wa NEST 360 ambao unatekelezwa Tanzania na Taasisi ya afya ya Ifakara kwa kushirikiana na Wizara ya afya pamoja na wadau mabalimbali ambapo Mkuu wa mkoa amewashukuru na kutoa rai kwa wadau wengine kuendelea kuisaidia sekta ya afya hapa nchini



Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa