-Amtaka Mkurugenzi kusimamia kwa karibu na kuchukua hatua Stahiki kuhusiana na hoja zinazotokana na upotevu wa fedha za umma
-Aelekeza Baraza la madiwani kurekebisha mienendo mibovu na kumsaidia Mkurugenzi kutekeleza majukumu yake vizuri
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa pongezi kwa Halmashauri ya jiji la DSM kufuatia kupata hati safi miaka mitano mfululizo huku akiwataka kuendelea kukusanya mapato zaidi kwa kuwa bado kuna baadhi ya vyanzo havikusanywi vizuri mfano chanzo cha Ushuru wa huduma (Service Levy)
Ameyasema hayo leo Juni 20,2023 wakati wa kikao maalum cha Baraza la madiwani la kupitia hoja za mdhibiti na mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika katika Ukumbi wa Arnatoglo Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila ametamka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji hilo kusimamia kwa karibu na kuchukua hatua Stahiki kuhusiana na upotevu wa fedha za umma, kutoa kipaumbele kwenye utekelezaji wa maagizo ya LAAC, kukijengea uwezo na kukitumia ipasavyo kitengo cha mkaguzi wa ndani na kujibu kwa wakati hoja zote za CAG
Aidha Mhe Chalamila ameelekeza Baraza la madiwani kuhakikisha linarekebisha mienendo mibovu katika Halmashauri na kumsaidia Mkurugenzi kutekeleza majukumu yake vizuri kwa kuwa uwezo huo wanao " namna peke ya kujipatia heshima kwa Mhe Diwani ni pale umma unapofarijika na utawala wake na si vinginevyo" Alisema RC Chalamila
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa