
-Achangia ushirika wa KKT Kimara Sadaka milioni 50.
-Asema Rais Dkt Samia anatuelekeza nyakati zote kufanya kazi kwa karibu na viongozi wa Dini
-Akubali mtoto mchanga iliyetoka mazingira hatarishi, anayelelewa na ushirika huo kubatizwa kwa jina lake
-Asema Shauku ya Mhe Rais Dkt Samia ni kuona Kila mtanzania anafanya vitu kwa Uhuru " Amani ikitoweka Vitu vingi hutoweka.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo Disemba 25,2025 ameshiriki ibada ya Sikukuu ya Christmas na waumini wa ushirika wa KKT Kimara Wilaya ya Ubungo Jijini humo.
Wakati wa ibada hiyo iliyongozwa na Mch. Mastai Mkuu wa Mkoa alipata wasaa wa kutoa salamu kwa waumini wa ushirika huo ambapo alisema yeye amekuja kusali hakutegemea kama angepata nafasi ya kusalimia hivyo anashukuru sana kwa kupatiwa heshima hiyo.
Aidha RC Chalamila amepongeza juhudi kubwa na ubunifu unaofanywa na mchungaji Mastai wa kuendeleza ushirika huo ni dhahiri kila kitu kinaonekana wazi idadi ya waumini ni kubwa lakini pia hata miundombinu ya ushirika huo imeendelea kuboreshwa ambapo ametoa sadaka ya milioni 50 ambayo anaamini itakwenda kuongeza nguvu katika ushirika huo.
Vilevile RC Chalamila amema Rais Samia anatuelekeza nyakati zote kufanya kazi kwa karibu na viongozi wa dini kwa kuwa viongozi hao ni nguzo muhimu katika ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa.
Sanjari na hilo RC Chalamila amemkubali mtoto mchanga ambaye ametolewa katika mazingira hatarishi, analelewa na ushirika huo na kubatizwa kwa Jina la Mhe Albert Chalamila ambapo RC Chalamila amepongeza ushirika huo kwa vitendo vya huruma vya kulea watoto wanatoka katika mazingira hatarishi "Hakuna mtoto wa mtaani, mtaa hauwezi kuzaa mtoto ni vema jamii itambue kuna umuhimu wa kulea watoto wanaoishi mazingira hatarishi ambao ni sehemu ya jamii" Alisema Chalamila

Mwisho RC Chalamila amesema shauku ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu ni kuona kila mtanzania anafanya vitu kwa Uhuru na Amani ikitoweka vitu vingi hutoweka hivyo ni muhimu kudumisha na kulinda amani ya taifa letu kamwe kilichotokea Oktoba 29 kisirudie tena

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa