Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ametembelea na kukagua ujenzi wa madaraja mbalimbali Jijini humo ikiwemo ujenzi wa daraja la Jangwani linalounganisha wilaya za Ilala na Kinondoni, daraja la mto mzinga wilaya ya Temeke pamoja na daraja la nguva na geti jeusi wilaya ya Kigamboni kwa lengo la kujionea kasi na viwango vya ujenzi wa miundombinu hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo RC Chalamila amesema Serikali imedhamiria kumaliza changamoto kwa wananchi hususani mafuriko ambayo yamekuwa yakikwamisha shughli za maendeleo za wananchi hivyo amewataka makandarasi kukamilisha miradi hiyo kwa wakati huku akiwataka wananchi kuunga mkono serikali kwa kutunza na kulinda miradi hiyo
Vilevile amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kutoa fedha nyingi za ujenzi wa miradi mbalimbali katika mkoa huo miradi ambayo inagharimu pesa nyingi kama vile mradi wa daraja la Jangwani unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 97, daraja la mto mzinga na barabara hadi kongowe shilingi bilioni 54, daraja la geti jeusi na daraja la nguva zaidi ya shilingi bilioni 9 kila moja.
Aidha RC Chalamila ametumia ziara hiyo kuzungumza na wananchi na kuwakumbusha kuwa Oktoba 29 mwaka huu ni siku ya uchaguzi mkuu hivyo wanapaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki kupiga kura kwa amani na utulivu bila kujihusisha na vitendo vya vurugu kwani ulinzi wa amani ya nchi ni juhumu la kila mtu na kwamba uvinjifu wowote wa amani hautovumiliwa.
Kwa upande wa Meneja wa TANROAD Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Razerk Kyamba ameeleza namna miradi yote ya ujenzi wa madaraja inavyoendelea na kusema kuwa ipo kwenye hatua nzuri licha ya kuwa baadhi yake ilichelewa kuanza kutokana na changamoto mbalombali ikiwemo mvua
Kwa upande wao wakuu wa Wilaya za Ilala na Kinondoni waliposhiriki ziara hiyo wamemshukuru Rais Dkt Samia kwa kuwezesha miradi hiyo ambapo wamesema ujenzi huo wa madaraja unakwenda kuwa suluhisho kwa wananchi dhidi ya athari za mafuriko
Hata hivyo wananchi waliojitokeza kumsikiliza mkuu wa Mkoa wameishukuru na kuipongeza Serikali kwa namna ambavyo ina inasaidia kutatua changamoto ya mafuriko kwa kujenga madaraja lakini wamemuomba Mkuu wa Mkoa kusaidia kupata huduma zingine ikiwemo kituo cha polisi eneo la mzinga na shule ya Sekondari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa