Mkuu wa Mkoa wa Dar es sSalaam Mhe Albert Chalamila amekukagua ujenzi wa daraja la Jangwani pamoja na ujenzi wa madaraja ya muda kwenye maeneo ya Kigogo na Mkwajuni yatakayotumiwa na wananchi kupisha ujenzi wa daraja la jangwani ambapo amewataka wakandarasi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati na kwa kuzingatia thamani ya fedha
Akizungumza leo Juni 27,2028 Jijini Dar es salaam akiwe kwenye eneo la ujenzi wa daraja la Jangwani RC Chalamila amesema ujenzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi hivyo amemtaka mkandarasi kufanya ujenzi huo kwa kiwango bora na ujenzi ufanyike kwa saa 24 ili ukamilike kwa wakati.
RC Chalamila amesema kuwa eneo hilo la jangwani limekuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi kila mvua zinaponyesha hivyo Rais Dkt Samia ametoa fedha za ujenzi huo na kwamba ujenzi wa daraja hilo utakua ndio suluhisho la adha hiyo na kusema kuwa hadi sasa serikali imeshampatia mkandarasi shilingi bilioni 14 kati ya shilingi bilioni 97 za kukamilisha mradi huo
Sanjari na hayo Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila ametumia nafasi hiyo kumtaka Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Meneja wa Tanroad Mkoa kuhakikisha uwanja wa mikutano eneo la jangwani unarejea ili uendelee kutumika kwenye shughuli za mikutano mbalimbali kama ilivyokuwa miaka iliyopita
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule waliposhiriki ziara hiyo wamemshukuru Rais Dokta Samia kwa kutoa fedha za ujenzi daraja hilo la jangwani pamoja na ujenzi wa madaraja ya muda kwenye eneo la kigogo na Mkwajuni ambapo wamesisitiza ujenzi huo kufanyika kwa haraka ili kumaliza adha kwa wananchi
Nae Meneja wa Tanroad Mkoa wa Dar es salaam Lazerk Kyamba amesema ujenzi wa daraja la jangwani unatanguliwa na ujenzi wa madaraja ya muda eneo la kigogo na mkwajuni yatakayotumiwa na wananchi wakati wa ujenzi wa daraja la jangwani ambapo pia kutakua na barabara ya dharura eneo la jangwani ambapo daraja la jangwani litagharimu shilingi bilioni 97 na ujenzi utafanyika kwa miezi 24
Ifahamike kuwa ujenzi wa daraja la jangwani ambao maandalizi yake yamefikia asilimia 7 unatanguliwa na ujenzi wa madaraja ya muda eneo la kigogo na eneo la mkwajuni utakaofanyika kwa miezi kumi madaraja ambayo yatatumika kupisha ujenzi mkubwa wa daraja kubwa la jangwani ambapo barabara hizo zitafungwa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa