-Atangaza kuanzia tarehe 20 hadi 22 /12/2024 Mkoa kwa kushirikiana na STAMICO kutakuwa na Kampeni kabambe ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia inayotokana na Mkaa uliotengenezwa na Makaa ya Mawe.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Disemba 17,2024 amehamasisha wakazi wa Mkoa huo kujenga tabia ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia ambayo ndiyo dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuona Watanzania wote na nchi zingine za kiafrika zinaachana na matumizi ya Nishati chafu ya kupikia badala yake zinatumia Nishati Safi ya Kupikia.
RC Chalamila amesema kwa muktadha huo Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirika la Madini STAMICO limeandaa kampeni kabambe ambayo itahamasisha wananchi kutumia Nishati safi ya kupikia ambayo ni mkaa uliotengenezwa kwa teknolojia kubwa inayotumia malighafi ya Makaa ya mawe.
Aidha Mkaa huo maarufu kwa jina la Rafiki Briquettes unaotokana na makaa ya Mawe umefanyiwa tafiti za kutosha za kisayansi pia umethibitishwa na TBS kuwa unafaa kwa matumizi ya kupikia na hauna athari zozote kiafya.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini STAMICO CPA Dkt Venance Mwasse amesma shirika limebuni teknolojia ya kutengeneza mkaa kwa kutumia malighafi ya makaa ya mawe ili kuunga mkono juhudi za Mhe Rais za matumizi ya Nishati safi ya kupikia kwa watanzania tena kwa bei nafuu ambayo kila mtanzania anaweza kuimudu hivyo amewataka watanzania kutumia fursa hiyo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa