-Ataka ubunifu na matumizi ya Teknolojia katika shughuli za ofisini, ukusanyaji wa mapato na utoaji huduma kwa wananchi
-Asisitiza kuibua miradi ambayo inaongeza ajira na kukuza uchumi wa watu.
-Atoa rai kujitokeza kwa wingi kupiga kura za Rais, Wabunge na Madiwani Octoba 29,2025.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg Abdul Rajab Mhinte kwa nyakati tofauti amekutana na watumishi wa Wilaya ya Temeke na Kigamboni ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha kwa watumishi wa wilaya zote za Mkoa huo.
Katibu Tawala Ndg Mhinte akiongea na watumishi hao leo Septemba 11, 2025 amepongeza kazi nzuri inayofanywa katika ukusanyaji wa mapato kwa kuwa Halmashauri zote mbili Temeke na Kigamboni zimevuka malengo ambapo amewataka kuendelea kuibua vyanzo vipya vya mapato ili ukusanyaji ukuongezeke zaidi.
Aidha amesisitiza matumizi ya teknolojia katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ofisini ukusanyaji wa mapato na katika kutoa huduma kwa wananchi.
Vilevile amezitaka Halmashauri hizo kubuni miradi ambayo itatoa ajira na kukuza uchumi wa wananchi katika maeneo yao pamoja na kuhakikisha wanasikiliza kero za wananchi kwa lugha za staha na kuzitatua pia kuhakikisha malalamiko ya wananchi yanapatiwa majawabu katika ngazi za chini pasipo kuruhusu malalamiko hayo kuja ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Sanjari na hilo amewataka Kigamboni kutumia vizuri fursa ya Ardhi waliyonayo kwa kuipima kisasa ili kuepuka misongamano na ujenzi holela, pia kwa upande wa Temeke kutumia vizuri fursa zinaotokana na uwepo wa viwanja vikubwa vya mpira kujipatia kipato zaidi.
Pia Ndg Mhinte ametoa rai kwa watumishi wote ndani ya Mkoa huo na wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo waliyojiandikishia kupiga kura ya Rais, Wabunge na Madiwani Octoba 29,2025 ili kupata viongozi wa kuwaletea maendeleo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa