Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda anapenda kuwakaribisha wananchi wa Mkoa huo kwenye Uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU itakayozinduliwa tarehe 07/09/2018 kwenye Viwanja vya Zakhem Mbagala.
Kampeni hiyo yenye Kauli Mbiu isemayo “PIMA, JITAMBUE, ISHI” inalenga kuongeza Utambuzi wa VVU na kuanza Dawa za Kupunguza Makali ya Virusi vya UKIMWI Mapema Iwezekanavyo.
Katika Uzinduzi huo Huduma mbalimbali za Afya zitatolewa bila malipo yoyote ambapo kutakuwa na Upimaji wa Virusi vya UKIMWI, Uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi, na Magonjwa yasiyoambukiza. Aidha,wananchi watapata nafasi ya Kuchangia Damu.
Huduma zote hizo zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 05/09/2018 hadi tarehe 07/09/2018 kuanzia saa mbili kamili asubuhi.
WITO: Wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam tunaombwa kujitokeza kwa wingi HASA WANAUME katika Kampeni hii ya FURAHA YANGU ili kuzijua vyema Afya zetu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa