Ibara ya 20(g) (ii) Kuelimisha Umma kuhusu fursa za kujiongezea Kipato kupitia Masoko ya Mitaji na Uwekezaji;
Mkoa umeweka mazingira mazuri na wezeshi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya sekta ya viwanda, biashara na masoko kwa lengo la uzalishaji wa ajira hasa kwa wafanyabiashara wadogo. Lengo ni kuwafanya wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga kuondokana na uchuuzi na kuwa wajasiriamali. Mkoa unalenga kuongeza idadi zaidi ya minada na magulio. Aidha, katika kuboresha maeneo ya biashara ndogo ndogo jumla ya masoko 8 yamekarabatiwa ambayo ni:-
Mkoa una mpango wa kujenga masoko ya kisasa katika maeneo ya Kisutu, Buguruni, Magomeni na Temeke stereo. Aidha, Mkoa kupitia Halmashauri zake pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Nchini (TanTrade) umetoa mafunzo kwa wafanyabiashara wapatao 3,142 ili kuwajengea uwezo juu ya stadi za biashara, ujasiriamali na upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya bidhaa zao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa