• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Ilala MC
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa azindua Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani

Posted on: May 31st, 2018

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara, mashirika na taasisi zote za Serikali na binafsi zianze kutumia nishati mbadala ili kuondoa kabisa matumizi ya kuni na mkaa.

“Wizara, taasisi na mashirika yote ya Serikali na binafsi pamoja na vikundi vya uzalishaji wanaotumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia au shughuli za uzalishaji waanze kutumia nishati mbadala ili matumizi ya mkaa yaishe na ikiwezekana yatoweke kabisa,” amesema.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Mei 31, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Mkaa ni Gharama: Tumia Nishati Mbadala.”

Waziri Mkuu amesema teknolojia bora ya uzalishaji wa mkaa mbadala ambayo ameiona kwenye maonesho hayo, ikuzwe na kusambazwa kote nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi waachane na matumizi ya mkaa wa kawaida na badala yake watumie mkaa-mbadala kwa lengo la kuhifadhi misitu na kupunguza uharibifu wa mazingira.

Ili kufanikisha matumizi ya teknolojia hiyo, Waziri Mkuu amesema vibali vya ujenzi wa majengo makubwa na taasisi kama shule, vyuo, hospitali navyo pia vianze kuzingatia ufungaji wa mifumo ya nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili kurahisisha upatikanaji na matumizi ya nishati mbadala katika taasisi na majengo makubwa.

“Wahandisi na wachoraji ramani za majengo waweke njia za kupitisha kwenye michoro yao ili ujenzi wa nyumba na majengo haya ukikamilika, watumiaji waweze kutumia teknolojia hiyo,” amesema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Mkoa wa Dar es Salaam ni lazima ubadilike na uachane na matumizi ya mkaa. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, mkoa huo unatumia tani 500,000 za mkaa kwa mwaka.

“Viongozi wa mkoa na wilaya ondokeni hapa na hili kama ajenda ya mkoa wa Dar es Salaam, mkaifanyie kazi na Wizara pia ifuatilie mmetekeleza kwa kiasi gani. Jitihada zilizofanywa na Jiji la Dar es Salaam kupitia kwa Mstahiki Meya, za kuanza kuwapa mtaji wajasiriamali hawa wanaotengeneza teknolojia mpya ni lazima ziigwe na nyie kwenye Manispaa zenu.”

“Meya ametoa fursa na amewaanzishia, na ninyi sasa endeleeni. Tengenezeni bajeti kupitia Mabaraza ya Madiwani na muwaunge mkono wajasiriamali wanaotengeneza haya majiko kwa kuwapa teknolojia hii kwenye maeneo yenu. Wanaotengeneza mashine za mkaa mbadala, wawezeshwe watengeneze mashine nyingi zaidi na zije kila Manispaa, ili kila Manispaa ianze kutumia teknonolojia hiyo kupikia,” alisisitiza.

Amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji la Dar es Salaam wafuatilie kwa karibu usambazaji wa teknolojia hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Yusuf Makamba amesema hali ya mazingira hapa nchini ni mbaya licha ya kuwa haionekani kwa haraka na watu waishio mijini.

“Hali ya mazingira nchini mwetu ni mbaya sana na inawezekana watu wanaoishi Dar es Salaam hawaioni kwa haraka kwa sababu mahitaji yao yote wanayapata sokoni na madukani,” alisema.

“Wenzetu wa mikoani na vijijii wanaotegemea mvua na udongo wenye rutuba wanataabika kwa sababu kipato chao kinaathirika kutokana na uharibifu wa mazingira,” alisema.

Alisema mazingira yanafungamana na utalii, kilimo, ufugaji, nishati, maji na kwamba maendeleo ya nchi pia yamefungamana moja kwa moja na mazingira. “Asilimia 90 ya Watanzania wanatumia kuni na mkaa kupikia lakini asilimia 70 ya mkaa wote unaozalishwa nchini Tanzania, unatumika jijini Dar es Salaam,” alisema.

Waziri Makamba alisema taasisi za Serikali kama vyuo, magereza, hospitali na shule zinaongoza kwa matumizi ya kuni na mkaa na hivyo kuchangia uharibifu mkubwa wa mazingira.

Akitoa mfano, alisema Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kina wanafunzi wapatao 30,000 na kinalazimika kuandaa milo mitatu kila siku.

“Chuo hiki kina migahawa tisa, kule nyuma kumejaa magogo ya kuni. Kuna mgahawa mmoja mdogo unatumia magunia 17 ya mkaa kwa siku, sasa huo mkubwa unatumia magunia mangapi?” alihoji.

Maadhimisho hayo yaliyozinduliwa leo, yataendelea hadi Juni 5, mwaka huu ambayo ni siku ya kilele. Pia wiki nzima kutakuwa na makongamano, midahalo na mjadala wa kitaifa.

Matangazo

  • Miradi 15 ya Kimkakati Awamu ya Pili Kutekelezwa February 06, 2019
  • Mkutano wa Mkuu wa Mkoa na Watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam 29/01/2019 January 28, 2019
  • Kuona Matokeo ya Kidato cha Nne 2018 bofya hapa January 24, 2019
  • Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anawatangazia wananchi wenye Matatizo ya macho kufika kwenye kambi ya macho iliyopo Mtaa wa Hindragand Posta kila Jumamosi na Jumapili kwa kipindi cha Miezi Miwili kupatiwa vipimo,matibabu na miwani bure. October 05, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makonda Awaagiza Wakuu wa Wilaya Kuhakikisha Ugawaji wa Vitambulisho Unamalizika Kabla ya Mwezi Machi

    January 29, 2019
  • RC Makonda Kumuenzi Askofu Pengo kwa Kuipa Barabara Jina lake

    January 26, 2019
  • RC Makonda Awahimiza Wananchi Kujipatia Bima ya Afya Ili Kujihakikishia Maisha Bora

    January 10, 2019
  • RC Makonda Awahakikishia Wanafunzi Waliofaulu katika Mkoa wa Dar es Salaam Kuendelea na Masomo Yao

    January 08, 2019
  • Tazama zote

Video

RC Makonda akiwasilisha utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa