Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ni moja kati ya Halmshauri za Manispaa tano zilizoko katika jiji la Dar es salaam nchini Tanzania. Mtazamo wa Halmashauri ni kuwa na jamii ambayo imewezeshwa kuendana na maendeleo ya kijamii, kiuchumi na Miundo mbinu. Malengo ya jumla ni kutoa huduma bora kwa jamii kwa kutumia rasilimali zilizoko kwa ufanisi, na kuwajengea uwezo , utawala bora na kuheshimu utawala wa sharia ambao utaboresha maisha ya jamii, Halmashauri inajipambanua kupitia uwajibikaji na utoaji huduma kwa watu.
Vyanzo vya Mapato vya Halmashauri hutegemea sana ushuru na kodi mbalimbli, vyanzo vikubwa vya mapato ni pamoja na kodi za Mabango, ushuru wa huduma za jiji, leseni za Biashara na kwa upande wa serikali kuu ni kupitia ruzuku inayotolewa katika maeneo maalumu kama Afya, Elimu, na Miundombinu. Vyanzo vya mapato havitoshelezi kukidhi mahitaji ya Manispaa ya kutoa huduma nzuri na bora, Halmashauri ya Manispaa imeweka nguvu kutoa huduma bora kwa umma na kutafuta fursa za uwekezaji.
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imepakana na Halmashauri ya wilaya ya Kibaha kwa upande wa kaskazini, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kusini mashariki na Halmashuri ya wilaya ya Kisarawe upande wa magharibi. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeunganishwa na Barabara nzuri na njia zingine za mawasiliano katika Jiji la Dar es Salaam na sehemu zingine za nchi . Barabara kuu zinazounganisha Halmashauri ni Barabara ya Morogoro, Barabara ya Mandela, na Barabara ya Sam Njoma.
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina kilometa za eneo 260.40, kutokana na Sensa ya watu mwaka 2012 Manispaa ina jumla ya watu 845,368 ambapo wanaume ni 409,149 na wanawake 436,219 lakini kwa makadirio ya idadi ya watu ya mwaka 2016 Halmashauri ya Manispaa ina jumla ya watu 1,031,349 ambapo wanaume ni 499,161 na wanawake 532,188.
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina hali ya hewa ya kiikweta ambayo kiujumla hali ya hewa ni ya joto na baridi kwa mwaka mzima, msimu wa joto zaidi ni mwezi wa kumi na mwezi wa tatu lakini mwezi wa tano na wanane ni baridi. Pia kuna misimu miwili ya mvua ambayo ni msimu mrefu na msifu mfupi, msimu mfupi ni kuanzia mwezi wa kumi na kumi mbili, msimu mrefu ni kati ya mwezi wa tatu na watano.
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina Tarafa mbili (2) Kibamba na Magomeni ambapo kuna kata kumi na nne (14) na mitaa tisini na moja (91) pia Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina majimbo mawili ya Uchaguzi, Halmshauri kimuundo inaongozwa na baraza la madiwani (Full Council) ambalo lina madiwani kumi na nne (14) wa kuchaguliwa na wabunge wawili (2) wa kuchaguliwa katika Majimbo.
Kujua zaidi kuhusu Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, bofya hapa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa