Kitengo Cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kina lengo la kutoa huduma za kitaalamu juu ya matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa Sekretarieti ya Mkoa, Aidha Kitengo hiki kinaongozwa na Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Mkuu ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni nyenzo muhimu, ambayo mchango wake ni mkubwa katika kuharakisha kufikiwa kwa Malengo ya Milenia ifikapo mwaka 2025. Kukua kwa teknolojia katika Mkoa wa Dar es Salaam, kuna mchango muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa kuhusu shughuli mbalimbali za utawala, sera na mipango kwa wakati mwafaka, hivyo kuwashirikisha wananchi moja kwa moja katika maamuzi yanayoathiri maisha yao. TEHAMA inatumika kila mahali na katika utoaji wa huduma za aina yoyote ile ikiwemo Elimu (Distant Learning, eLibrary), matibabu (telemedine), biashara (eCommerce, eBanking, nk),Ukusanyaji wa mapato, uongozi/utawala (eGovernace) n.k.
Kutokana na kuingia kwa utandawazi, dunia sasa imekuwa kama kijiji kimoja tena kidogo sana, kwani mawasiliano yamekuwa yakiboreshwa siku hadi siku na kuwa rahisi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa