Utangulizi
Jiji la Dar es Salaam lipo kati ya latitudo nyuzi 6 hadi 7 na longitudo kati 39.45 kwa upande wa Mashariki na nyuzi 39 kwa upande wa magharibi, Kusini mwa ikweta na upande wa magharibi, Kusini na Kaskazini. Jiji linapakana na Mkoa wa Pwani, upande wa Mashariki linapaka na Bahari ya Hindi. Jiji la Dar es Salaam lina eneo la ukubwa wa kilomita za Mraba zipatazo 1,800; kati ya hizo, kilomita za mraba 1,350 ni eneo la nchi kavu ikijumuisha visiwa vinane vilivyopo katika eneo la bahari ya Hindi. Jiji hupata joto la wastani wa kati ya nyuzi 25 hadi 33 na mvua katika misimu miwili ya vuli ambayo ni miezi ya Oktoba Desemba na Masika ambayo huanza miezi ya Machi Mei.
Idadi ya watu
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka ... Jiji lina idadi ya watu ..... ambapo kati yao wanaume ni ......na wanawake ni........
Historia ya Halmashauri ya Jiji
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa inaliongoza Jiji kutoka mwaka 1961 mpaka mwaka 1972, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizivunja Halmashauri zote nchini na kuwa chini ya Usimamizi wa Serikali Kuu (Madaraka Mikoani)
Serikali Kuu ilizirudisha Serikali za Mitaa Nchini, Chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) na. 8 ya mwaka 1982, ambapo Halmashauri ya Jiji ilianza kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa wananchi kuanzia mwaka 1983.
Mwaka 1996 Serikali Kuu iliivunja Halmashauri ya Jiji na kuunda Tume ya jiji la Dar es Salaam, kwa Tangazo la serikali Na. 110 na 111 ya tarehe 28 Juni mwaka 1996.
Tume ya jiji ilifanya kazi kwa kipindi cha miaka minne, ambapo mwaka 2000 Serikali iliunda mamlaka nne za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na. 8 ya Mwaka 1982, kama ilivyo rekebishwa kwa sharia na. 6 ya mwaka 1999.
Utawala
Kiutawala Jiji limegawanyika katika Halmashauri sita za Serikali za mitaa ambazo ni:
• Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
• Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
• Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
• Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
• Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
• Halmashauri ya Manispaa ya Kigambomi
Mstahiki Meya ni Kiongozi Mkuu na Mkurugenzi wa Jiji ni Mtendaji Mkuu kwa upande wa Serikali za Mitaa.
Kujua zaidi kuhusu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bofya hapa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa