-Ataka wale ambao hawajajiandisha hadi sasa kutumia vizuri siku chache zilizobaki kujiandikisha
-Atangaza kufanya ziara ya kimkakati usiku wa manane katika wilaya zote za Mkoa
-Asema Serikali inatarajia kusaini mkataba wa ujenzi wa daraja la Juu Jangwani.
-Atangaza tamasha kubwa la mapishi kwa kutumia nishati safi DSM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amesema mwenendo wa uandikishaji daftari la mpiga kura katika Mkoa huo linaendelea vizuri Ikiwa leo ndio ukomo wa uongozi wa wenyeviti wa Serikali za mitaa Serikali katika Mkoa huo ambapo amewataka wananchi mkoani humo kutumia vyema muda mchache uliobaki kuweza kujiandikisha kwenye daftari la wakaazi ili kushiriki uchaguza wa kupata viongozi wapya wa Mitaa.
Akizungumza leo Oktoba 19, 2024 jijini Dar es salaam na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa huo Mhe Albert Chalamila amesema zoezi hilo linakwenda vizuri huku akitoa rai kwa wale wote ambao bado hawajajiandikisha watumie muda uliobaki wa siku ya kesho kujiandikisha kabla zoezi halo halijafungwa
Aidha Chalamila ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mchakato wa ujenzi wa wa bonde la msimbazi na daraja la jangwani ambapo amesema Oktoba 22, 2024 Serikali kupitia wizara ya TAMISEMI inatarajia kusaini mkataba wa ujenzi huo pamoja na ujenzi wa baraba zinazoambatana na mkataba huo
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam katika kuhakikisha wananchi Mkoani humo wanapata huduma stahiki kutoka kwa watumishi wa umma kuanzia Oktoba 22,2024 anatarajia kuanza kufanya ziara nyakati za usiku kwenye maeneo mbalimbali ya huduma za umma ikiwemo hospitali na ujenzi wa barabara za mwendokasi ambazo ujenzi wake unapaswa kufanyika saa 24.
Sanjari na hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wananchi wa Mkoa huo na maeneo ya jirani kushiriki katika Tamasha la mapishi kwa kutumia nishati safi litakalofsnyika Novemba 02,2024 kwenye viwanja vya biafra kinondoni ikiwa ni katika kumuunga mkono Rais Dokta Samia kwenye kampeni yake ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa