- Asema maandamano yanachelewesha uchumi, husimamisha biashara, hufifisha utoaji huduma za afya pia kuleta taharuki
-Asistiza vijana kutumia muda kuelewa tija ya maendelezo na ubia wa Bandari na sio kufanya maandamano
- Akemea upotoshwaji wanaosema nchi imeuzwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa onyo kali kwa kikundi cha watu wanaopanga kufanya maandamano kupinga Serikali kufanya maendelezo na Ubia wa Bandari ya Dar es Salaam.
RC Chalamila amesema hayo leo Juni 19, 2023 Ofisini kwake Ilala Boma wakati akiongea na Waandishi wa Habari.
Mhe Albert Chalamila amesema anauhakika watu hao hawajui wanachokifanya, pia hawajapitishwa vizuri kufahamu Mkataba wa uendelezaji na ubia wa Bandari vilevile hawajui tija ya makubaliano ya uendelezaji wa Bandari hivyo Serikali iko tayari wakati wowote kueleza tija ya maendelezo na Ubia wa Bandari hiyo.
Aidha RC Chalamila amesema maandamano siko zote hayana faida yoyote zaidi ni kuchelewesha uchumi, kusimamisha biashara, kufifisha huduma za afya na kuleta taaruki kwa jamii ambazo zitarudisha nyuma maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.
Hata hivyo RC Chalamila amewataka Vijana au kikundi cha watu wanaopanga kufanya maandamano kutumia muda huo Kipitia Mkataba wa Maendelezo na Ubia wa Bandari ili kujua nia njema ya Serikali na tija ya maendelezo hayo
Sambamba na hilo RC Chalamila amekemea upotoshwaji unaofanywa na watu wanaosema nchi imeuzwa hata siku moja Rais hawezi kuuza nchi Rais ameapa kulinda nchi na kuwaletea Maendeleo wananchi wake na siku zote Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akipambana kuleta maendeleo na maisha bora kwa kila mtanzania
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa