• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Atinga kwa Kushtukiza Tabata Kimanga

Posted on: June 10th, 2024

-Akagua maendeleo ya barabara ya Tabata Mazda hadi Kimanga 

Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 10 ,2024 amefanya ziara ya kushtukiza kukagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mazda kimanga Km 3.7 Wilaya ya Ilala. 

RC Chalamila amefanya ukaguzi huo kufuatia ahadi aliyoitoa kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa kuongea na wananchi wa eneo hilo alioufanya Tabata Kimanga Mei 30,2024.

Mhe Albert Chalamila amemtaka mkandarasi anayejenga barabara hiyo kuongeza kasi ili mradi ukamilike kwa wakati, wananchi wa maeneo hayo waweze kuitumia katika shughuli zao za kila siku za kujiletea kipato. 

Aidha RC Chalamila amesema Rais Dkt Samia ameelekeza nguvu kubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali hapa nchini hususani Mkoa huu, “Niwatake makandarasi waliobahatika kupata kazi kufanya kazi kwa weledi kuzingatia muda na thamani ya pesa “ Alisema RC Chalamila Vilevile RC Chalamila ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuelimishana juu ya kutoziba mifereji ya maji taka pia kutotupa taka ovyo ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kuziba mifumo ya maji taka 

Sanjari na hilo RC Chalamila amewataka wananchi kutokuwa na shaka kuhusu kusua kusua kwa ujenzi wa barabara hiyo ambapo amesema atakuwa anafuatilia kwa karibu maendeleo ya barabara hiyo pale atakapoona kuna shida atachukua hatua stahiki mara mmoja 

Mwisho RC Chalamila ametoa rai kwa wananchi kuendelea kulinda amani ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa ndicho kitovu cha uchumi wa nchi, Diplomasia na mambo mengine mengi yenye maslahi mapana kwa nut mmoja mmoja, Taifa la Tanzania, na mataifa mengine Duniani

Matangazo

  • DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 July 17, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA WA DARASA LA SABA MEI, 2025 July 18, 2025
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais Dkt Samia Suluhu Kuzindua Kituo cha Uwekezaji Ubungo - EACLC Aug 1,2025

    July 30, 2025
  • Tanzania Mwenyeji Ufunguzi wa "African Nations Championship" CHAN

    July 21, 2025
  • RC Chalamila Akutana na Meya wa Jiji la Dallas-Marekani

    July 21, 2025
  • RC Chalamila Aelekeza Kuundwa Kamati ya Kutatua Mgogoro wa Ardhi Sahara-Mabibo

    July 19, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa