-Amshukuru Rais Dkt Samia kwa kutoa pesa nyingi zinazowezesha utekelezaji wa miradi hiyo
-Ataka usimamizi mzuri wa miradi kwa kuzingatia viwango na thamani ya pesa
-Asikiliza kero za wananchi wa Kata ya Saranga na kuzipatia majibu papo hapo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila leo April 09,2025 amefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Kibamba wilaya ya Ubungo na kuagiza miradi hiyo kujengwa kwa viwango na kuzingatia thamani ya fedha, ambapo ameagiza miradi hiyo kukamilika kwa wakati
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa jengo la mama na mtoto kwenye kituo cha afya cha Mpiji Magoe RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa nyingi ambazo zinawezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo ambapo amesema ni muhimu kufanya ujenzi wa miradi unaozingatia thamani ya fedha, miradi inayoweza kudumu kwa miaka mingi na ujenzi ukamilike kwa wakati ili kumaliza adha kwa akina mama na watoto
Akiwa kwenye mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Goba Kulangwa RC Chalamila amesisitiza suala la ulinzi na usalama hasa nchi ikiwa inaelekea kwenye uchaguzi mkuu hivyo ameagiza kukamilishwa kwa ujenzi wa kituo cha polisi cha Tegeta A
Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Juma Japhari Nyaigesha amewataka wananchi na wafanyabiashara kuto kukwepa kulipa kodi kwani ndio chanzo cha kupata fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo vituo vya afya huku Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Mpiji Magoe Hereswida Cosmas akieleza maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo la mama na mtoto amesema ujenzi unaendelea vizuri na utakamilika kwa wakati.
Aidha Katika ziara hiyo wilayani Ubungo RC Chalamila pia ametembelea na kukagua mradi wa maji wa kibamba, pamoja na kukagua mradi wa shule ya sekondari goba kulangwa
Mwisho RC Chalamila amefanya mkutano wa hadhara Kata ya Saranga eneo la ofisi ya Serikali ya mtaa na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ikiwemo ubovu wa barabara, changamoto ya TASAF, Maji, kusuasua kukamilika kwa ujenzi wa zahanati ambapo ameahidi kabla ya kufika ijumaa ya wiki ijayo pesa tasilimu shilingi milioni 100 zitakuwa zimeletwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo hata hivyo ametolea ufafanuzi kero zingine kwa kuwahakikishia Rais Samia yuko kazini Changamoto zote zitatuliwa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa